ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 21, 2015

AIRTEL YAZINDUA MNARA WA HUDUMA ZA MAWASILIANO WILAYANI ARUMERU ARUSHA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika kijiji cha Nduruma, wilayani Arumeru Mkoani Arusha , akishuhudia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala akitoa msaada wa vitabu Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi , Hamad Boay , wakati wa uzinduzi wa huduma manara wa huduma za mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika kijiji cha Nduruma, wilayani Arumeru Mkoani Arusha. Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu ni pamoja na sekondari za Nduruma na Singisi wilaya Arumeru
Press Release Airtel yazindua Mnara wa huduma za Mawasiliano Arumeru wilayani Arusha.
 * Zaidi ya wakazi 25,000 kufaidika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi
 * Shule mbili za sekondari zapatiwa msaada wa vitabu 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma za mawasiliano ya simu za mkononi katika kijiji cha Nduruma wilayani Arumeru mkoani Arusha na kuwawezesha wakazi zaidi ya 25,000 kupata huduma za mawasiliano. 

Katika uzinduzi huo , Airtel pia ilitoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule mbili za sekondari za Nduruma na Sing'isi, vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 4 Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala alisema"

 Uzinduzi huu ni mwendelezo wa dhamira yetu unaoenda sambamba na mipango ya serikali ya kutoa huduma za mawasiliano kwa kila mtanzania. 
Leo tunayofuraha kuwawezesha wakazi wa vijiji vya Samaria, Majimoto na Maroran kupata huduma za mawasiliano za uhakika, zenye ubora na za gharama nafuu huku tukiwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa ufanisi zaidi" "Tunaamini huduma hizi za mawasiliano zitachangia katika kuboresha shughuli za kiuchumi zikiwemo ufugaji, kilimo pamoja na biashara ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi. 

Sasa wakazi wa Nduruma wamewezeshwa kupata habari muhimu kupitia simu zao za mkononi wakati wotote na kwa urahisi zaidi" Majwala aliongeza kwa kusema" Sambamba na uzinduzi wa huduma za mawasiliano pia tumeweza kutoa vitabu vya sayansi kwa shule mbili za sekondari wilaya hapa ili kuwawezesha wanafunzi na jamii kupata elimu bora. 

Tunaamini vitabu hivi pamoja na huduma hizi za mawasiliano zitachangia kwa kiasi kikubwa k kubadili maisha ya wengi na kuwawezesha watanzania na wakazi wa hapa kuzifikia ndoto zao". 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato ambaye ndiye aliyezindua mnara huo na kutoa vitabu kwa shule za sekondari alisema" tunayofuraha kupata huduma za mawasiliano kutoka Airtel hapa Nduruma pamoja na vijiji vya jirani. 

Hii ni nafasi ya pekee kwa wakazi wa hapa kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kutumia mawasiliano haya katika kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kijamii" "Serikali itaendelea kuwaunga mkono Airtel katika jitihada zao za kuhakikisha inatanua wigo wa huduma za mawasiliano na kufikia maeneo mengi hususani yaliyo pembezoni mwa nchi. 

Nawapongeza sana kwa juhudi hizi na kuwaasa wakazi wa hapa kutumia fulsa hii katika kujiendeza na kuleta maendeleo" Kwa upande wake, Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi , Hamad Boay alisema" Tunashukuru sana Airtel kwa kutupatia msaada huu wa vitabu ambao utaboresha uwiano wa vitabu na idadi ya watoto shule ambapo hapo awali kitabu kimoja kinatumika na wanafunzi watano, msaada huu utaboresha uwiano ambapo kwa sasa mwanafunzi mmoja atatumia kitabu kimoja. 

Tunaahidi kuvitumia vizuri na kuvitunza lakini zaidi wanafunzi wetu watafanya vizuri kimasomo na kutoa wanasayansi bora shuleni hapa."

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.