ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 23, 2015

AIRTEL YAZINDUA OFA YA LUKU.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa Habari  leo katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel  nchini kupata Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel na (Kulia) Steven Kimea Meneja wa Airtel Money.
 Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kujipatia nyongeza ya Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, anayefwata  kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika ofisi ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Airtel yazindua ofa ya LUKU
·         Wateja kupata unit za luku za bure pale watakaponunua umeme kupitia huduma ya Airtel money
Dar Es Salaam, Juni 23 2015 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money
Ofa hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel Money
Akiongea kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na  mahitaji na mwendendo wa maisha ya watanzania.  Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi  kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme. leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za Luku za ziada za bure”.
Aliongeza kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya  mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine nyingi.  Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.