Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu.
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa.
Sheria ya filamu ya mwaka 2012 inasema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja lakini sivyo inavyofanyika.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.