ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 24, 2015

AMBASADA LU YOUQING NA MHE .MASELE WAZUNGUMZA JUU YA MKUTANO WA JUKWAA LA VIONGOZI VIJANA AFRIKA NA CHINA

Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu Youqing (kulia) akiwa na Naibu waziri Ofisi ya makamu wa rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele ambao wamekutana leo  kuzungumzia mkutano wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AMBASADA LU YOUQING NA MHE .MASELE WAZUNGUMZA JUU YA MKUTANO WA JUKWAA LA VIONGOZI VIJANA AFRIKA NA CHINA

20/ Machi/ 2015, Dar es salaam, Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu Youqing na Naibu waziri Ofisi ya makamu wa rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele wamekutana leo  kuzungumzia mkutano wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.

Jukwaa hilo la viongozi vijana lenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi, linatarahiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo atahutubia wageni waalikwa kutoka zaidi ya nchi 40, huku mambo mbalimbali yakiwasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa kwenye jukwaa hilo.

Akiongea na waandishi wa habari katika Ubalozi wa watu wa china hapa nchini, Dr. Lu Youqing alitoa maoni yake juu ya mkutano huo sambamba na kutaja baadhi ya maeneo ambayo viongozi vijana wa China wangependa kujifunza wakati wa mkutano huo.

“Tunafahamu kwamba China ni mwekezaji mkubwa sana kwenye nchi za Afrika na kila siku tuona biashara za aina mbalimbali zinazofanyika baina ya bara la Afrika na nchi ya China. Tanzania ni nchi mojawapo Afrika ambayo China imewekeza zaidi na kupitia mkutano huu ninaamini kuwa urafiki wetu pamoja na uchumi kati yetu utaendelea kukua zaidi”

Tofauti na urafiki mzuri ulio baina ya nchi hizi mbili Balozi Lu Youqing aliongeza kuwa uchumi wa Tanzania unaridhisha na unaendelea kukua kila siku, huku akitaja kuwa ndio sababu kuu ya kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu wa kimataifa.

Kwa upande wake Naibu waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo alisema…“Dhumuni kubwa la mkutano huu ni kuimarisha uhusiano mzuri ulipo kati ya China na Afrika lakini pia ni fursa muhimu kwa vijana wafanyabiashara kupanua mawazo yao na kufungua milango ya kibiashara kati ya Afrika na China”. Mhe. Masele alitaja baadhi ya maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kama Fedha na uwekezaji, Kilimo, Madini, Uchumi na Biashara.

Tunatarajia ugeni wa zaidi ya vijana 200, Afrika ina vijana wengi ambao tunaamini kupitia mkutano huu wataweza kujifunza fursa mbalimbali za kujenga maisha yao ya baadae iwe ni kiuchumi au siasa” …aliongeza Masele.
Alimalizia kwa kukishukuru chama cha mapinduzi kwa kuonyesha ushirikiano thabiti wakati wa kipindi hiki amabacho wapo kwenye mchakato wa maandalizi ya mkutano huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.