ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 24, 2015

STARS YATUA MWANZA TAYARI KUIKABILI MALAWI KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA

Wachezaji wa Timu ya taifa la Tanzania Taifa Stars wakiwasili hoteli ya Lakairo mara baada ya kutua na ndege ya Shirika la ndege la Fast Jet asubuhi ya leo.
Mbwana Samatta ni mmoja wa wachezaji wa Stars walio wasili hii leo.
Stars.
Mshauri wa Rais Masuala ya Ufundi Peregrinius Lutayuga, akizungumzia maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mchezo wake dhidi ya Malawi utakao chezwa dimba la CCM Kirumba Mwanza, jumapili ya March 29, 2015. 
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora akizungumza na baadhi ya waandishi wa habariza michezo kuhusu mkoa ulivyojiandaa kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema na kuibuka na ushindi dhidi ya Malawi, mchezo utakao chezwa dimba la CCM Kirumba Mwanza, jumapili ya March 29, 2015. 
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA

Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars tayari imewasili jijini Mwanza kwa mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Malawi.

Stars imetinga jijini humo ikiwa na wachezaji 18 tu ambapo wengine sita toka Yanga Africans wamebaki jijini Dar es salaam wakisubiri kumalizia mchezo wa kiporo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu utakao chezwa Jumatano.

Deogratius Munish, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Hassan Dilunga na Simon Msuva watajiunga na wenzao walioko jijini Mwanza siku ya Alhamisi. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.