Na
Mwandishi Wetu.
ZAIDI ya wachoma Nyama na wamiliki wa
Bar 143 wa Temeke, Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo ya uchomaji nyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya
Safari Nyama Choma 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo hayo,
Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Manase Mwasha alisema lengo la Kampuni ya Bia Nchini (TBL)
kwenye mashindano ya Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa
kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu
viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma.
Alisema Manase, wachoma nyama katika baa za mikoa yote
inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa
mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.
Tumezingatia maombi ya
washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya
uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache
zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.
Aliendelea kufafanua Jaji Mkuu Manase, washiriki watapimwa ujuzi
wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya
mbuzi na nyama ya kuku.
Manase Mwasha alisema katika mafunzo hayo alisisitiza
zaidi vitu muhimu watakavyoangalia katika fainali za kumpata mchoma nyama bora
wa mkoa kama usafi, vifaa vya kufanyia kazi, joto maalumu lakuhifadhi nyama na
joto maalum la uchomaji nyama.
Tayari mikoa ya Mbeya, Mwanza, Aresha na Kilimanjaro
wameshapewa elimu hii ya Uchomaji Nyama ili kuelekea katika fainali za kumpata
bingwa wa kila mkoa katika mikoa shiriki ya mashindano ya Safari Lager Nyama
Choma 2015.
Mikoa inayoshiriki fainali za mashindano ya Safari Lager
Nyama Choma 2015 ni Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Bingwa wa mkoa katika kila mkoa atajinyakulia zawadi ya
kikombe na pesa taslimu milioni moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.