Tumekwisha sikia mashauri mbalimbali yakirindima toka pande na pande yakihusu kesi tofauti tofauti za watu kushitakiwa kuwatendea sivyo wanyama hata ndege, iwe ni katika jinsi ya kuwafuga, kuwasafirisha toka sehemu moja hadi nyingine na kadhalika. Lakini sijasikia shtaka kuhusu mnyama huyu Nguruwe ambaye ni maarufu kwa jina la 'Kitimoto' aka 'Mdudu' au wabishi wengine humuita 'Mbuzi Katoliki'.
Likija suala la ubebaji (usafirishaji), ufugaji hata uchinjaji mnyama huyu hupitia wakati mgumu sana na huchinjwa/kuuliwa kwa style ya kinyama zaidi kuliko wanyama wote ambao ni kitoweo cha binadamu ingawa kwa wengine ni haramu.
Swali ni jeh mnyama huyu hana mtetezi au ama..... Chunguza mjomba utabaini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.