ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 24, 2015

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WALIOKUWA WANAKAA CHINI WAPATIWA MADAWATI

VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI 
WANAFUNZI wa shule ya msingi mafizi iliyopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu  ya kukaa chini kwa muda mrefu kutokana na uhaba wa madawati wamepatiwa msaada wa madawati 100 na shirika la umeme Tanesco  kwa ajili ya kupunguza kero hiyo.

Shule hiyo ya msingi ambayo kwa sasa ipo katika wakati mgumu imepatiwa msaada huo wa madawati kwa ajili ya kuungua juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira ambayo ni rafiki ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Wanafunzi hao wakizungumza mara  baada ya kupokea msaada hu wa madawati 100 kutoka Tanesco akiwemo Kela Kesi Bolasi julias pamoja na Jumaidi Shabani walisema kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kutokana na kuandikia wakiwa chini ya sakafu.

Walisema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ya madawati kunachangia kwa kiasi kikubwa kutofanya vizuri katika masomo yao kwani wakati mwingine wanajikuta wanaumwa mafua kutokana na kuwepo kwa vumbi.

“Kwa kweli sisi wanafunzi wa shule ya msingi mafizi kwa kipindi cha muda mrefu baadhi yao tulikuwa tunasomea chini ya sakafu lakibi kutokana na msaada huu wa madawati kutoka Tanesco utaweza kutufanya tusome katika mazingira ambayo ni rafiki kwetu hivyo tunawapongeza sana kwa msaada waliotupatia,” alisema wanafunzi hao.

Kwa upande wao Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe pamoja Mkejina Mnyanga pamoja na Kaimu afisa elimu shule za msingi Narsisa Lihepanyama walisema kuwa msaada huo katika shule hiyo  utaweza kuongeza chacu zaidi ya ufaulu kwani wanafunzi hao wataweza kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwa upande wao.

Naye Meneja mwandamizi wa Shirika la umeme Tanesco kanda ya dare s Salaam na Pwani Mahende Mugaya mara baada ya kutoa msaada huo katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo ambayo yalifanyika katika shule hiyo na hapa  alikuwa na haya ya kusema kuhusina na mikakati ya tanesco katika kusaidia katika sekta ya elimu hapa nchini hapa naweka bayana.

Mgaya alisema kwamba mimikakati ya Tanesco ni kuhakikisha inaunga juhudi za serikali katika kuboresha setka ya elimu hasa katika shule zilizopo vijijni  ambazo zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinawafanya wanafunzi kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki kwa upande wao.

SHULE  hiyo ya msingi ambayo  ina idadi ya wanafunzi 260 ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati na kupelekea wanafunzi zaidi ya 100 kujisomea wakiwa chini ya sakafu hali ambayo ilisababisha wengine kupata ugonjwa wa mafua kila kukicha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.