Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha... |
Washindi wa kwanza wa mbio za makasia wa Kisiwa cha ukerewe kikundi cha Nichoraus Ngoroma wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki. |
NICHORAUS NGOROMA MABINGWA MBIO ZA BALIMI MITUMBWI UKEREWE.
Na Mwandishi wetu, Kagera.
KIKUNDI cha Wanaume wa piga kasia cha Nichoraus Ngoroma Kisiwa
cha
Ukerewe kimeibuka na ubingwa katika fainali za mashindano ya mbio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi
Extra Lager zijulikazokama “Balimi Boat Race 2014”
na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/=
pamoja na kuwakilisha Kisiwa hicho kwenye fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Kapina Kagari ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
600,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika fainali za Kanda
jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha
Athumani Malemo ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Mashauri Saidi ambacho kilizawadiwa Shilingi
400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Asante Robert, Ladsilaus Musimu, Benedicto Aniseti, Gervas Kulwa, Simon Fundi na Silvari Sasieli.
Upande wa Wanawake kikundi cha
Muhate Mwocha kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi
700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda
jijini Mwanza.
Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Mlanzi Mussa ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=, washindi watatu ni kikundi cha Joyce Makalu ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Beatrice Kalomba ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Pili Masitu, Adventina Elias, Jesca Jose, Veronica Machumu, Juliana Petro na Maria Mabagara.
Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Mlanzi Mussa ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=, washindi watatu ni kikundi cha Joyce Makalu ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Beatrice Kalomba ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Pili Masitu, Adventina Elias, Jesca Jose, Veronica Machumu, Juliana Petro na Maria Mabagara.
Akizungumza wakati wakukabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,
Mery Tesha kwanza
alitoa shukrani kwa Kampuni ya bia nchini (TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager
ambao ndio wadhaminiwa mashindano hayo na kuwaomba waendelee kudhamini kwani yanaleta hamasa umoja na udugu kati yetu kuiachiliambali afya na kipato kinachopatikana kama zawadi mara baada ya mashindano.
Tesha alisema washindi waliopatikana wakaiwakilishe vyema Ukerewe na wahakikishe wanarudi na ushindi na
wale ambao hawakupata nafasi ya kushinda wajiandae kwa mashindano mengine mwakani.
Tesha alimaliza kwa kuwaomba zawadi walizopewa wakazitumie kwa maendeleo yao kwani huo ni mtaji tosha kwa mtu anayeweza kujishughulisha.
Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi
Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika Desemba 6,
mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.