Wakichezesha droo ya kwanza ya Ndovu Golden Experience. |
DROO YA KWANZA YA NDOVU SPECIAL MALT
CHINI YA “NDOVU GOLDEN EXPERIENCE” YAFANYIKA KUSAKA WASHINDI WA KUTEMBELEA HIFADHI ZA SELOUS.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, Jumatatu 17-11-2014
Ndovu Golden Experiencekupitia kinywaji chake cha Ndovu Special Malt, leo
hii imechezesha droo yake ya kwanza ya kupata washindi watakaoweza
kutembelea hifadhi za Selous.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Bi. Pamela Kikuli alisema kuwa “Washindi hao watajipatia fursa ya kutembelea hifadhi hizo na tunaamini
kuwa fursa hii itawapa hamasa kubwa ya kujifunza zaidi na kuendelea kumlinda Mnyama Tembo na hifadhi
za Wanyama kwa ujumla” Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa
Tanzania, ila, utalii mkubwa unaofanyika
hapa Tanzania ni wa wageni kutoka nchi za nje. Hivyo basi tunaamini kuwa kwa
kuendeleza kampeni yetu hii ya ‘Ndovu Golden Experience’ inayoendeshwa kupitia
namba zilizo chini ya kizibo cha bia ya Ndovu Special Malt, itawa fursa muhimu
sana watanzania ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyo ndani ya nchi yetu.
Gharama
za malazi, chakula pamoja na usafiri zitakuwa chini ya kampeni ya “Ndovu Golden experience” kupitia kinywaji
chake cha Ndovu Special Malt. Washindi hao wataongeza idadi
katika takwimu ya Wazawa wanaotembelea hifadhi za Wanyama Nchini.
Alimalizia
kwakusisitiza kuwa,watumiaji wote wa
kinywaji cha Ndovu Special Malt kushiriki kwa wingi katika shindano hilo kwa kutuma namba zilizofichwa kwenye kizibo kwenda 15499 au kwa njia ya tovuti www.ndovuspecialmalt.com/goldenexperience.
Hifadhi za Selous ziko Kusini mwa
Tanzania, ukubwa wa kilometa za mraba 54,600.Ina Wanyama wakubwa kama vikle
Tembo, Mbwa Mwitu, Nyati, Kiboko, Mamba, Simba na aina 450 za ndege warukao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.