MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo eneo la Shams, jijini Arusha
Kisa cha kujiua kwakwe kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine eneola Mbauda wakati akitoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Kwa Mrombo.
Alikutwa na mautihayo majira ya kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku ndani ya baa hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kuwatishia kwa bastola madereva wa bodaboda waliokuwa wamemzingira eneo la ajali na kisha kuwaponyoka kwa kasi na gari lake aina ya Nissan Navara.
"Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzingira wakanywea, akatumia mwanya huokuwakimbia na moja kwamoja alifika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa...
"Ingawa alionekana alikotoka alikunywa kidogo, Alipofika Arusha Raha alikunywa pombe mbili kali aina ya Valuu (Valeur) na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale madereva wa bodaboda". Anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili hewani, lakini bila ya watu hao kutishika, ndipo alipoamua kujimiminia risasi.
Habari zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wakiwa katika harakati ya kupiga simu Polisi walishtukia wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa amejitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.
kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa Ofisi ya Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio hilo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.