ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 28, 2014

MTOTO ALIYETENGWA KWA ULEMAVU NCHINI TANZANIA AWEKA HISTORIA YA KUWA WA MILIONI 1 KUFANYIWA UPASUAJI MDOMO SUNGURA

Mratibu wa Taasisi ya Smiletrain hapa nchini, Mahamoud Ally (katikati) akiwa amembeba mtoto Osawa Simba (9) wa kijiji cha Bigegu Kata ya Kitale Wilaya ya Bunda mkoani Mara ameweka historia ya kuwa mtoto wa milioni moja duniani katika Namba ya waliofanyiwa upasuaji wa kurekebishwa ulemavu wa mdomo "Mdomo Sungura" aliozaliwa nao na sasa amerejeshwa kwao baada ya kupona kabisa na kupokelewa na jamii kijijini kwake. Kulia ni mama na kushoto ni baba wa mtoto huyo Owiti Simba. 
Mtoto Osawa Simba sasa anatasamu vyema.
Kulia ni mama na kushoto ni baba wa mtoto Osawa Simba wakati wakizungumza na wageni walio watembelea. 
Makazi ya familia ya Bwana na Bibi Owiti Simba inategemea ghala hili lililo upande wa kulia katika himaya yao na kushoto ni sehemu ya nyumba yao. 
Mratibu wa Taasisi ya Smiletrain hapa nchini, Mahamoud Ally akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwenye himaya ya Bwana Owiti Simba iliyoko katika kijiji cha Bigegu Kata ya Kitale Wilaya ya Bunda mkoani Mara, ambapo mtoto Osawa (9) ameweka historia ya kuwa mtoto wa milioni moja duniani katika Namba ya waliofanyiwa upasuaji wa kurekebishwa ulemavu wa mdomo "Mdomo Sungura" aliozaliwa nao. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY
Jirani wa familia akisimulia jinsi jamii ilivyokuwa ikimnyanyapaa mtoto Osawa aliyezaliwa akiwa na mdomo uliopasuka (Mdomo Sungura), tofauti ya sasa na yazamani. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY

Mratibu wa Taasisi ya Smiletrain hapa nchini, Mahamoud Ally (kulia) na bwana Owiti Simba wakiwa na mtoto Osawa Simba (katikati) wa kijiji cha Bigegu Kata ya Kitale Wilaya ya Bunda mkoani Mara aliyeweka historia ya kuwa mtoto wa milioni moja duniani katika Namba ya waliofanyiwa upasuaji wa kurekebishwa ulemavu wa mdomo "Mdomo Sungura" aliozaliwa nao na sasa amerejeshwa kwao baada ya kupona kabisa na kupokelewa na jamii kijijini kwake.
Picha ya pamoja familia, ndugu, majirani na marafiki. 
Wadau wa Taasisi ya Smiletrain wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya bwana Owiti walipofika kumtembelea mtoto wa milioni moja duniani katika Namba ya waliofanyiwa upasuaji wa kurekebishwa ulemavu wa mdomo "Mdomo Sungura" aliozaliwa nao na sasa amerejeshwa kwao baada ya kupona kabisa na kupokelewa na jamii kijijini kwake..
Wadau wa Taasisi ya Smiletrain wakimuaka mtoto Osawa
Himaya.
Kushoto Mratibu wa Taasisi ya Smiletrain hapa nchini, Mahamoud Ally akiagana na mama Osawa.
MTOTO ALIYETENGWA KWA ULEMAVU NCHINI TANZANIA AWEKA HISTORIA YA KUWA WA MILIONI 1 KUFANYIWA UPASUAJI MDOMO SUNGURA
MTOTO Osawa Simba (9) wa kijiji cha Bigegu Kata ya Kitale Wilaya ya Bunda mkoani Mara ameweka historia ya kuwa mtoto wa milioni moja duniani katika Namba ya waliofanyiwa upasuaji wa kurekebishwa ulemavu wa mdomo "Mdumo Sungura" aliozaliwa nao na sasa amerejeshwa kwao baada ya kupona kabisa na kupokelewa na jamii kijijini kwake.

Awali mtoto huyo alionekana kutengwa na watoto wenzake kwa kuzaliwa na kilema cha kupasuka mdomo wake ambapo kinywa chake kilionekana kubaki wazi wakati wote na baada ya kufanyiwa upasuaji sasa amepokelewa kwa shangwe hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji na kuonekana kupona ulemavu huo.

Hatua hiyo imetokana na wazazi wa mtoto huyo kurejea kijijini hapo baada ya mtoto wao kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam kwa ufadhili wa Taasisi ya Smiletrain ya Marekani akiwa ni mtoto wa milioni moja kufadhiliwa gharama ili kufanyiwa upasuaji wa marekebisho ya mdomo uliosababisha awali kutengwa na wanajamii.

Akizungumza na waandishi wa habari, Baba mzazi wa mtoto huyo Owiti Simba alieleza kwamba tangu alipomzaa mtoto huyo alionekana kutengwa na jamii kutokana na kuzaliwa akiwa na kilema cha mdomo (kupasuka) hali ambayo ilipelekea majirani kushindwa kushirikiana naye huku watoto wakimkimbia kutokana na mwonekano wake wa utofauti.

“Awali nilipompeleka Hospitali ya DDH wilayani Bunda mwaka 2005 na kushauriwa na Daktari kuwa umri wa mtoto huyo bado ni mdogo hivyo hataweza kufanyiwa upasuaji hadi atakapokuwa mkubwa kidogo sikukata tamaa, mara ya pili nilipompeleka ndo nikaelezwa kuna watu watakuja kumuona na kweli watu hawa walikuja na kuandaa utaratibu wa kumfanyia upasuaji” alisema.

Simba alisema kutokana na kuwa na hali duni ya kiuchumi ilisababisha kuomba msaada zaidi kwa mdaktari hadi alipopata msaada wa kutoka kwa wawakilishi wa Taasisi hiyo ya Smiletrain ya Marekani ambapo walifika kijijini Bigegu na kutathimini mazingira magumu anayoishi ikiwa ni pamoja na kupiga picha mazingira hayo kisha kuahidi kutoa ufadhili wa kiasi cha Sh milioni moja ili mwanaye afanyiwe upasuaji. 

“Nashukuru upasuaji huu umeonekana kuwa na mafanikio na sasa mtoto wangu ameanekana kupona kabisa na kurudisha muonekano wa kibinadamu na sasa amekuwa akicheza na wenzake na hata kusoma darasani bila kutengwa kama awali kutokana na ulemavu wa mdomo na amekuwa na bidii ya kwenda shuleni kuliko ilivyokuwa wakati hajafanyiwa upasuaji” alisema.

Kwa upande wake mratibu wa Taasisi ya Smiletrain hapa nchini, Mahamoud Ally alisema kuwa tangu kufanyiwa upajuaji kwa mtoto huyo imekuwa ni faraja kwa taasisi hiyo kutokana na namba iliyofikiwa kuwa ya milioni moja tangu taasisi hiyo kufadhili gharama za watoto katika maeneo ya mataifa mbalimbali duniani kwa mafanikio makubwa.

“Huyu ni mtoto wa milioni moja kufanyiwa upasuaji tokana na jina lake kuonekana kwenye usajiri ambao ilionekana kuwa Namba ya milioni moja dhidi ya watoto mbalimbali waliofanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa au kupata ulemavu wa mdomo kupasuka (Mdomo Sungura) kwenye maumbire ya mwili duniani kote ikiwemo Kenya, India, China na Marekani”alisema.

Ally alisema kuwa baada ya upasuaji huu na kuendelea vizuri kwa Osawa, amewataka wazazi kutowaficha watoto wanaozaliwa vilema na badala yake wawapeleke Hospitali ili kuwezesha watoto hao kupata matibabu na upasuaji, huku akiwasihi kuachana na tabia ya kukimbilia imani za kishirikina kuwa zimekuwa zikisababisha watoto wengi kukosa msaada wa matibabu na kupoteza maisha.

Mratibu huyo alisema kwamba mbali na kumtembelea kila wakati mtoto huyo kuona maendeleo yake pia Taasisi ya Smileterain itakakikisha inamsaidia kupata elimu kwa kuwezesha kulipia gharama zote kutokana na mtoto huyo kuwa balozi wa milioni moja aliyepatiwa msaada wa kulipiwa gharama ya upasuaji kutokana na familia yake kushindwa kufanya hivyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.