WAREMBO WA MISS
UNIVERSE TANZANIA 2014 WAANZA KAMBI
Warembo wa
Miss Universe Tanzania 2014 wameanza
rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Golden Tulip Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na
fainali ya Miss Universe Tanzania 2014 itakayofanyika
tarehe 02 mwezi Octoba.
Miss
Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo
ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa
na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji
mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema usaili wa mwaka
huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania na warembo zaidi ya 70
walisajiliwa kwa mashindano haya.
Kambi ya
Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa mitano ya
Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam, pamoja na
mrembo mmoja kutoka Zanzibar.
Pamoja na
zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss
Universe Tanzania 2014 atapata fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali na
kufanya kazi za kijamii. Pia kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4 sasa, mshindi
atapewa nafasi (scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi
sasa washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako
New York masomoni.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa
kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia
amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa
kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata
James ,2010 Hellen Dausen , 2011 Nelly
Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface ambaye ndiye anakabidhi
taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na Insignia, MeryLight , Golden Tulip, Compass
Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Missie Popular blog,
Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys Entertainment (TZ) Ltd na New York Film Academy.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mwanakombo Salim: 0655441165.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.