Airtel yaanzisha mradi wa huduma kwa jamii ujulikanao kama TUNAKUJALIKampuni Airtel Tanzania leo imetangaza kuanzisha mpango wa huduma kwa jamii utakaowashirikisha wafanyakazi wake kujitolea na kushiriki katika kuchangia na kusaidia jamiii nchini.
Mpango unategemea kuanza wiki hii unashirikisha wafanyakazi kutoka katika vitengo mbalimbali utawawezesha wafanyakazi hawa kuandaa shughuli zitakazowawezesha kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia shule mbalimbali ambazo zina mahitaji muhimu katika maeneo mbalimbali nchini.
Mradi huu umezindulia rasmi na Kitengo cha huduma kwa wateja ndio kitakuwa cha kwanza kushiriki ambapo wameandaa burdani ya musiki itakayowashirikisha magwiji mahiri wa muziki nchini King KKii and Banana Zoro inayotegeme kufanyika siku ya jumatano tarehe 3 septemba 2014 katika viwanja vya ofisi ya Airtel.
Wafanyakazi wa Airtel na watu
mbalimbali kutoka nje wamealikwa kushiriki na kiasi cha pesa
kitakachopatikana kitaenda kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum Tanga.
Akiongea kuhusu mpango huu Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema” katika kushiriki kutatua changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii wafanyakazi wa Airtel wameona ni muhimu kuanzisha mpango huu maalumu wa kusaidia jamii.

Airtel kupitia mpango wake wa huduma
kwa jamii umeonelea ni vyema kutenga siku 14 mahususi kwa wafanyakazi
kupata muda wa kusaidia jamii. Hivyo tutakuwa na shughuli mbalimbali
kuanzia sasa zitakazofanya na wafanyakazi katika kukusanya fedha na
kisha kufatiwa na siku 14 za kutoa misaada wa jamii zinazotegemea
kuanza rasmi mwakani mwezi wa tatu. Lengo letu ni kuhakikisha
tunazifikia shule 10 na kuzisaidia kwa sasa na leo tunachukua
nafasi hii kuwaalika wafanyakazi wetu na jamiii kutuunga mkono na
kushirikiana nasi”.
“Baadhi ya shule zitakzofaidika na mpango huu ni pamoja na shule ya Msingi Pongwe Tanga itakayojengewa darasa, shule ya msingi ya kumbukumbu Dar es salaam itapatiwa msaada wa viti na meza kwa darasa la watoto wa masomo ya awali, shule ya sekondari Ndala watapewa vifaa vya ofisi kwa wafanyakazi , uhuru mchanganyiko watanunuliwa mashine ya Braile pamoja na vifaa vya kufundishai na shule ya msingi kimara watapatiwa tanki ya kuhifadhi maji.
"Nia yetu ni kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi na jamii kwa ujumla" aliongeza Mbando.

Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia sekta ya elimu nchini mpaka sasa zaidi ya shule 1000 zimeweza
kufaidika na vitabu kupitia mradi wa Shule yetu” wiki iliyopita
Airtel imetangaza zaidi ya shule 30 zitakazofaidika na misaada ya vitabu kwa mwaka huu wa 2014 na leo kupitia wafanyakazi wake Airtel inaendelea kuwafikia watu wengi zaida na jamii nzima kwa ujumla nchini.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.