Na
Mwandishi Wetu.
FAINALI
za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival
2014” Mkoani Mwanza kikundi cha Mwanalyaku cha chenye makazi Magu kimefanikiwa kuwa mabingwa wa Mkoa wa Mwanza na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi
600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi
cha Bujora cha Magu pia ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi
cha Utandawazi cha Ukerewe ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Wadonho cha Sengerema ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi
300,000/=.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na kikundi
cha Mwanza Sanaa na nafasi ya sita ilikwenda kwa kikundi cha
Ngoma Buhongwa ambavyo vilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 150,000/= kila kikundi.
Jumla yaVikundi 6, vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Mwanza ngazi ya Mkoa kwa Mwaka
2014.
Akizungumza na kwanya kati tofauti Meneja matukio wa
Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano
ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni
sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra
Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.