ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 6, 2014

UZINDUZI WA PEPSI KOMBE LA MEYA KWA MKOA WA MWANZA WATIKISA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na mamia ya wahudhuriaji wa uzinduzi wa Pepsi Kombe la Meya uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akipiga penati ya kuashiria ufunguzi wa Pepsi kombe la Meya 2014 ambapo golini alisimama muhasisi mwenyewe wa mashindano Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula. Ndikilo alifanikiwa kuukwamisha mpira huo wavuni.
Kabla ya uzinduzi timu 22 washiriki wa mashindano hayo zilifanya paredi la utambulisho. 
Hiki ni kiatu cha dhahabu ambacho atakitwaa mfungaji bora wa Pepsi Kombe la Meya ikiwa ni sambamba na kitita cha shilingi laki mbili.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameambatana na meza kuu kusalimia wadau wa timu 22 shiriki wa Pepsi Kombe la Meya 2014, anayefuata ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye ndiye mwasisi wa mashindano hayo Stanslaus Mabula, Mweyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza Jackson Songora na wadau wengine.
Sasa ni zamu kwa timu ya Igoma Fc.
Mhe. Mama Hewa akisalimiana na timu ya Wanahabari, anayefuata ni diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha.
"Michezo ni furaha...tehe....teh!!!!!"
Isamilo Fc katika picha ya pamoja kabla ya kutinga dimbani kupambana na Mkolani Fc.
Mkolani Fc.
Katika mchezo huo Mkolani Fc waliibuka kidedea kwa kuibamiza Isamilo Fc bao 3-1.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na mamia ya wahudhuriaji wa uzinduzi wa Pepsi Kombe la Meya uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. 


Patashika langoni  mwa Mkolani Fc.
Umakini wa mashabiki michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014.
Baada ya mchezo kumalizika Balozi wa Pepsi kwa wasanii Kala Jeremiah alipiga show.
Kala Jeremiah na hisia zake.
Wow...
Muda wa kuwapa tano mashabiki.
Kala Jeremiah akimtambulisha kaka yake katika game ya muziki wa kizazi kipya H. Baba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.