|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR |
|
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR |
|
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR |
|
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR |
|
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR |
|
Kongamano. |
|
Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi. |
|
Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi. |
KONGAMANO hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha jana Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara.
Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.
Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.