ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 6, 2014

SERENGETI FIESTA 2014 YATEMBELEA RADIO WASHIRIKA NA WASHIKAJI VITAA VYA MWANZA

Mtangazaji wa kipindi cha Michano Time kupitia radio Passion Fm ya jijini Mwanza Philbert Kabago (kushoto) akifanya mahojiano na wadau wa Kamati ya Serengeti Fiesta 2014, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Sebastian Maganga (katikati) na Mratibu wa shughuli za uhamasishaji Dj Mully B (kulia).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Sebastian Maganga akizungumza ndani ya kipindi cha 'Michano Time' ambapo amewasisitiza washiriki wa kinyang'anyiro cha shindano la Serengeti Dance la Fiesta kuwahi hiyoo kesho (alhamisi ya tarehe 7/08/2014) kwaajili ya mchakato mzima.

SERENGETI DANCE LA FIESTA:
Washriki lazima wawe kwenye kundi la kuanzia watu wanne mpaka nane, Na wawe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, Kujiandikisha ni kuanzia jana (5/08/2014) uwanja wa Nyamagana kuanzia saa kumi jioni mpaka saa kumi na mbili jioni, fainali za dance la Fiesta ni alkhamisi (7/08/2014)  kuanzia saa tano asubui pale jembe ni jembe na mshindi atajishindia sh Milioni moja. 

SERENGETI SUPER NYOTA DIVAZ:
Hili ndo shindano lilitoa wasanii wengi wachanga ambao kwa sasa wamekuwa wakubwa na wamepata mafanikio, ambao wote wanatokea hapahapa Mwanza, Hapa unamzungumzia Young Killer aliyekuwa mshindi wa ujumla mwaka juzi pamoja na Mo Music aliyeishia nafasi ya tatu mwaka jana hapa mwanza wote hawa wanafanya vizuri kwa hivi sasa,

Kwa zaidi ya Miongo miwili Super Nyota ilikuwa ikitoa nafasi kwa jinsia zote mbili kushiriki yaani wavulana na wasichana, lakini mwaka huu tumebadili na kuamua kutoa nafasi kwa wasichana pekeake, ambae yoyote Yule ambae ni msichana na ana kipiaji ndo atapata nafasi kushiriki , ambapo mshindi atapelekwa Dar Es Salaam kwa ajili ya kushindanishwa na washiriki wengine toka katika Mikoa mingine.

Zoezi la kujiandikisha litahitimishwa kesho eneo la tukio Jembe Beach Malimbe saa 4 kabla ya kuanza kwa usaili, ambapo fainali zake zitaanza siku hiyo hoyo mida ya saa tano asubuhi, mshiriki lazima awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.

KITAANI:-
Baada ya kutoka studio za redio washirika , 'Amshaamsha' ya Serengeti Fiesta ilijikita katika uwanja wa Nyamagana, pichani prizenta wa XXL Adam Mchomvu aka Baba Jonii (kulia) akipiga mastori na raia wa kitaa, hukupale kati Mratibu wa shughuli za uhamasishaji Dj Mully B akifuatilia yalokuwa yakijiri. 
Hapa raia wa kitaa alikuwa akiangusha maneno ya hisia...kinowma nowma!!
Mtu wako wa nguvu Millard Ayo damu damu na watu wake.
Prizenta wa XXL Mchomvu akizungumza na Producer D. Classic (mwenye t.shirt white) 
Baba la baba na watu wake....!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.