ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 12, 2014

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MITINDO KWA NJIA YA SIMU KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNIFU MAHIRI AFRIKA.

Mbunifu nguli wa mitindo Afrika, Mustafa Hassanali akizungumza na wageni waalikwa kuhusiana na huduma mpya ya kuwa karibu naye kwa mashabiki wa mitindo kupata taarifa zake kupitia simu zao za  mkononi za Airtel  kwa kupiga *148*82# na moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hiyo na kutozwa shilingi 90 za kitanzania kwa siku.
Press Release
Airtel yazindua huduma mppya ya mitindo kwa njia ya simu kwa kushirikiana na  Mbunifu  Mahiri Afrika.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, imeshirikiana na mbunifu wa mitindo Afrika ,Mustafa Hasanali katika kusheherekea miaka 15 ya mafanikio yake makubwa katika sekta ya mitindo.

Mustafa Hassanali amefanya maonyesho katika miji 27 katika nchi 18, na kugusa maisha ya watu mbali mbali  kwa njia tofauti. Na anaendelea kuwa maarufu katika sekta ya mitindo nchini na Afrika kwa ujumla.

Ushirikiano huo kati ya Airtel na Guru wa mitindo  Tanzania na nje ya Tanzania, utawezesha wateja wa Airtel na washabiki wa mitindo kuwa karibu  zaidi na ulimwengu wa mitindo kwa kupata habari mbali mbali na za kisasa kupitia simu zao za mikononi.

Akiongea kuhusu muungano huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba, alisema “mitindo ni moja kati ya vipengele muhimu katika maisha yetu, zikiwemo nguo, vifaa na vyombo mbalimbali. Kila mtu anataka kupendeza na kujihusisha na mitindo ya kisasa. Ila , hivi sasa upatikanaji wa habari na huduma za mitindo ni mgumu sana. 

Hivyo Airtel tumekuwa wa kwanza katika kuwapatia wananchi huduma hii kupitia simu zao za mkononi itakayowasaidia kupata habari mbali mbali za mitindo kwa ujumla . Huduma hii inajulikana kwa jina la “Airtel Fasheni”. Tunaamini kuwa , huduma hii itawasaidia wateja wetu wote ambao wangependa kupata habari mbali mbali na kuwafikia wabunifu wa mitindo ili kupata ushauri na pia kununua bidhaa zao.”

Mustafa Hassanali, mbunifu mitindo mahiri Afrika alisema , “ Airtel fasheni ni huduma ya kipekee ambayo wateja wa Airtel wanaweza kuipata mahali popote na wakatii wowote kwa kupiga *148*82#. Huduma hii ni Tsh.90 kwa siku.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.