ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 12, 2014

MUIGIZAJI NGULI ROBIN WILLIAMS AIAGA DUIA

 Simanzi limetanda nchini Marekani kufuatia kifo cha muigizaji Nguli Robbin Williams. Salamu za rambi rambi zimeendelea kumiminika kufuatia kifo cha Williams, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka sitini na sita. 

Polisi wanaamini kwamba Robin amejiua yeye mwenyewe akiwa nyumbani kwake katika mji wa Carlifonia.Gwiji wa utengenezaji filamu Steven Spielberg amefafanua kwamba Williams alikua na kipaji cha namna ya kipekee katika sanaa ya uchekeshaji na alikua ni muigizaji maarufu sana.




Naye Rais wa Marekani Barack Obama alimuelezea Williams kwamba katika uchekeshaji wake alikua akigusa maisha ya watu. Robin Williams katika uhai wake alikua maarufu sana na mcheshi katika kipindi cha runinga kilichojulikana kama 'Mork and Mindy' kabla hajageukia katika tasnia ya filamu kama ya Good Morning Vietnam na pia alikua ni mshairi na mashairi yake yalikua ya kuvunja mbavu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.