Upakuaji ukiendelea. |
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu (kushoto) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael wakisaidizana kufanikisha shughuli hiyo ya makabidhiano. |
Mafuta kwa Kituo. |
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na wadau wa Airtel. |
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema. |
Shukuran...Aksante!! |
Kampuni ya za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari katika vituo vinavyolea watoto waliopo katika mazingira magumu nchini.
Kupitia mpango huu Airtel imetoa msaada wa chakula kwa kituo cha Sharif Saidi Al-Bath kinacholea watoto yatima kilichopo Nyegezi Majengo Mapya Jijini Mwanza
Akiongea wakati wa kukabithi msaada huu , Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana Raphael Daudi alisema” Airtel Kwa kutambua changamoto nyingi zinazozikumba jamii tumeonelea ni vyema katika mfungo huu wa ramadhani kutenga muda wa kutembelea na kutoa msaada kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini. Leo tumetembelea kituo hiki cha Sharif Saidi Al-Bathi na kuwapatia msaada wa chakula ambacho kitawasaidi hata baada ya mwezi wa ramadhani.
lengo letu ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla, husasani watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha tunarudisha faida tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia shughuli zetu za huduma kwa jamii kila mwaka.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath bwana Alhaji Hussein Mussa Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu, tumefurahi sana na kuona kumbe watanzania wenzetu na mashirika mbalimbali wanaunga mkono jitihada zetu katika kuhakikisha tunawalea na kuwasomesha watoto yatima. Kituo chetu bado kina mahitaji mengi hivyo natoa wito kwa taasisi zingine kujiunga na kuendelea kusaidia kituo chetu na vituo vingine nchini
Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo hiki wameishukuru Kampuni ya Airtel kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyotoa na kuyatala makampuni mengine kuiga yale yaliyofanywa na kampuni hiyo.
Vituo vingine vitakavyopata msaada kutoka Airtel ni pamoja na New Hope Family group-Temeke, Al-Hidaya children’s Home-ilala, Irishad Madrasah-Mbezi kwa Msuguri (kinondoni), Kiboa orphanage-Arusha na Heartfelt orphanage care Mbeya
Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath chenye watoto Yatima zaidi ya 50 kilichopo Mwanza tayari kimepokea msaada kutoka Airtel mwishoni mwa wiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.