HAIJAWAHI kutokea tangu nchi hii kupata uhuru mwaka 1961 kwa wananchi wa mji Tarime kushuhudia mechi ya fainali kombe la dunia kati ya timu za
Ujerumani na Argentina nchini Brazil kupitia TV kubwa tatu katika eneo moja bure zilizowekwa katikati ya stendi ya mabasi na kupata huduma ya vyoo bure mjini humo.
Wakizungumza wakati wa kushuhudia fainali hiyo, baadhi ya mashabiki
wamempongeza mjasiliamali Gisuruli
Mwihechi maarufu "Six" ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Six Office Solution and Computer Ltd. kwa kuwapunguzia makali ya kulipia
gharama za kuangalia michuano hiyo tangu zilipoanza fainali hizo.
Chacha Mwita mkazi wa mjini Tarime amesema kwamba
Mwihechi ameonyesha uzalendo kwa jamii iliyokuwa haina uwezo wa kulipia katika
mabaa pia migahawa ili kuangalia mechi moja kwa shilingi kati ya 1000 na 2000
jambo lingewanyima uhondo wa wananchi wengi kushudia mipambano hiyo ya fainali
za kombe la dunia.
“ mimi ningelitumia elfu sitini hapo sijanywa bia
lakini vijana wengine wangelazimika kuiba ndizi, mifugo ili kuuza wapate
fedha za kulipia viingilio, lakini pia alionyesha ungwana pale alipoamua kulipia gharama za vyoo ili kutolewa bure kwa wananchi na mashabiki katika kipindi chote cha kuanza kwa mashindano ya fainali hizo kama wangelipa viingilio na huduma hiyo ya vyoo wasingeweza kuwa na fedha za ziada za kupeleka mahitaji muhimu majumbani
mwao.” Alieleza Juma Thomas.
Kwa upande wake mkurugenzi Mwihechi alipozungumza na
gazeti hili alisema kwamba aliamua kusaidia wananchi kwa kujua kuwa kombe la
dunia ni muhimu hivyo akaamua kuwasaidia watizame michuano hiyo bure kwa pamoja
ili kusaidia kunusuru uakali wa maisha kwa kujinyima kupoteza kipato kidogo
walichonancho kukipeleka kwenye viingilio.
“ Nimelifanya haya si kwa sababu za kuwania
uongozi wa kisiasa bali kuwaunganisha wananchi wenye tofauti zao kiujumla pamoja na kuwapatia fursa ya kujifunza zaidi kupitia fainali hizo, mchezo wa soka unaongoza kwa kuwa na mashabiki ni soka lakini pia mimi nikiwa mzaliwa wa Tarime nilikumbuka kusaidia ndugu zangu wasiokuwa na uwezo ili nao wapate kushuhudia michuano hii bure na kubeba sehemu ya gharama hizo .” Alisema.
Mwihechi amewapongeza wananchi wa Mji na Wilaya hiyo ya Tarime kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha mwezi mmoja walichokuwa wakishuhudia mashindano hayo ya fainali za kombe la dunia bila kufanya vurugu au vitendo vya uhalifu, kurushiana maneno yenye lugha za kuudhi au kejeli baina ya mtu na mtu bali kuwa wamoja ili kutoa fursa kwa wananchi kuangaliahusiano naiofauti zao ili kuondokana pia na lindi la
umaskini kwa vijana kuendeleza vipaji vya soka kupitia runinga wakati timu 32 zilipoanza kumenyana hadi kupatikana bingwa wa kombe hilo 2014 timu ya Taifa ya Ujerumani.
Wito kwa wazaliwa wananchi wa Wilaya ya Tarime waliojaliwa kupata mali na kuukwepa umasikini wakumbuke kurudi na kusaidia wananchi wenzao kila mmoja kwa nafasi yake kwani itakumbukwa wilaya hiyo inazo changamoto nyingi za kijamii ikiwemo za Afya, Elimu, Maji, Mifugo, Uvuvi, Miundombinu ya Barabara, Michezo, Mawasiliano na Nishati ya Umeme na Uwekezaji katika sekta zote za kutoa huduma kwa jamii ili kuwezesha kupiga hatua za maendeleo zaidi pia kushirikiana na viongozi wao waliowachagua kuwawakilisha na wale wa serikali hakika hakuna litakaloshindikana kuiona Wilaya hiyo ikichanua na kuzonga mbele kimaendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.