Emenike alichangia pakubwa mechi hii. |
Nigeria
ilisajilia ushindi wake wa kwanza katika kombe la dunia katika kipindi cha
miaka 16 ilipoilaza Bosnia-Hercegovina 1-0 katika mechi yao ya pili ya kundi F.
Ushindi
wa mwisho wa Super Eagles ilikuwa ni mwaka wa 1998.
Mfungaji bao hilo Peter Odemwinge naye alifunga bao lake la kwanza la kombe la dunia baada ya miaka minne.Bao hilo la pekee lilifungwa na Peter Odemwinge kunako dakika 29 ya kipindi cha kwanza alipopokea pasi safi kutoka kwa Emenike .
Bao
hilo hata hivyo litajadiliwa kwa upana na marefu ikizingatiwa kuwa wachezaji wa
Bosnia walimlalamikia vikali refarii wa mech hiyo wakisema kuwa Emenike alikuwa
ameponda nahodha wa Bosnia Spahic kabla ya kummegea odemwinge pasi murwa.
Odemwinge akiifungia Nigeria bao dhidi ya Bos- Hez. |
Aidha
msaidizi wa refarii atakumbukwa kwa kumnyima bao safi Edin Dzeko aliyesemekana
kaotea lakini picha za runinga zilionesha haikuwa kweli na hivyo Bosnia
watelekea nyumbani wakijua vyema kuwa mechi hiyo ingeishia sare ya Moja kwa
moja isingalikuwa ni msaidizi wa refarii.
Kipa wa
Super Eagles Vincent Enyeama alikuwa na wakati mgumu kumzima Dzeko aliyefanya
mashambulizi katika muda wa majeruhi katika mechi hii.
Nigeria
sasa itakabiliana na Argentina katika mechi yao ya mwisho ya makundi .
Kufuatia
Ushindi huo Super Eagles imejikita katika nafasi ya pili ikiwa na alama 4 mbili
nyuma ya vinara Argentina ambao walilazimika kufanya kazi ya ziada kuilaza Iran
bao 1-0.
Iran ni
ya tatu huku Bosnia ikiyaaga mashindano haya baada ya mechi yao ya mwisho dhidi
ya Iran.
Nigeria
itafuzu kwa mkondo ujao iwapo itashinda ama kutoka sare na Argentina katika
mechi yao ya mwisho.
Vilevile
Super Eagles itafuzu iwapo Bosnia itailaza Iran.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.