· *Ni njia salama, ya uhakika na yenye viwango vya tozo nafuu zaidi sokoni*
Wateja wa Airtel wameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia bidhaa na huduma zake husisani huduma ya Airtel Money kuwa ni bora na salama nchini
Huduma hii ijulikanayo kama "Hatoki Mtu Hapa" inawawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bila makato kwa kununua kifurushi cha wiki au cha mwenzi cha Bure Pack na pia kuwawezesha wateja kutuma pesa kwa nusu gharama ukilinganisha na ziwango vinavyotozwa sokoni. Ambapo kwa sasa Airtel ndio kampuni inayotoza viwango vya chini vya miamala ya pesa nchini.
Wakiongelea kuhusu huduma za Airtel, wateja wa Airtel jiji Dar es saalam walisema" tunafurahishwa na hufuma ya Airtel money kwani inatuhakikishia usalama wa pesa zetu
"huduma ya Airtel Money inamgusa kila mtanzania kwani kutuma na kupokea pesa ni kitu kisichokwepeka katika maisha yetu ya kila siku, na kama tunavyofahamu si salama sana kutembea na kiasi kikubwa cha pesa mfukoni,
huduma ya Airtel Money ni mkombozi wa huduma za kifedha na usalama wa pesa zetu katika maisha ya sasa. Pamoja na huduma hii kutoa usalama pia inatoza viwango vya gharama zaidi yaani Nusu gharama inaleta unafuu na kutupatia ziada ambayo inatuwezesha kutumia pesa hizo kufanya mambo mengine ya muhimu" alisema Finora Fokasi mmoja wa wateja wa Airtel Money.
Kwa upande wake baadhi ya mawakala wa Airtel Money walithibitisha kuwa 'Hatoki mtu hapa' imepokelewa vizuri na wateja kwani tumeona ongezeko la wateja katika vituo vyetu wakija kufanya miamala ya pesa . Hii nikutokana na ukweli kwamba mteja ambaye angetozwa shilingi 7000 kutoa pesa kupitia mitandao mingine sasa kwa kupitia huduma ya Airtel Money "Hatoki Mtu Hapa" anatozwa shilingi 3500, niwazi kabisa kuwa punguzo la bei limekuwa kivutio hivyo kuongeza idadi ya wateja wa Airtel Money"alisema Paulo Msangi Mkazi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.