ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 15, 2014

NYANZA BOTTLING CO. LTD YAFANYA UZINDUZI WA PROMOSHENI YA KOMBE LA FIFA LA DUNIA 2014.

Meneja masoko wa Nyanza Bottling company LTD ambao ni watengenezaji wa bidhaa na soda za Coca Cola jijini Mwanza akizungumza kwenye uzinduzi wa Promosheni ya Shamrashamra kuelekea fainali za kombe la FIFA la Dunia ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.
Tukio hili linalogusa kwa namna ya kipekee watumia wa Coca Cola na watanzania kwa ujumla likifanyika kwa kutambua umuhimu wao ambapo nyanza Bottling Itaendesha Kampeni Kanda ya Ziwa itakayowawezesha wapenzi wa soka na wananchi kwa ujumla kuhamasika na fainali zenyewe, lakini pia kujishindia zawadi kem kem.
Ni maelfu ya zawadi ikiwa ni pamoja na TV bapa za inchi 32 aina ya Sony, fulana maridadi na mipira yenye nembo ya Kombe la FIFA la Dunia 2014. Hakuna shaka zawadi hizi zitaleta shangwe kubwa kwa wale watakao bahatika kuzipata.
Baadhi ya wadau wa vitengo kampuni ya bidhaa za soda za Coca Cola Mwanza.
Kwa kuwa lengo kubwa la promosheni hii ni kombe la Dunia Coca Cola imeona itatoa zawadi ya tiketi ambapo washindi wa tiketi hizo watapelekwa nchini Brazil kwenda kujionea wenyewe mchezo wa robo fainali za kombe la Dunia, huku ikiwalipia washindi hao gharama zote kuanzia tiketi za kwenda na kurudi, chakula, malazi na tiketi za kuingia uwanjani kutizama mchezo huo.
Wapenzi wa soka dunia nzima sasa wanajiandaa kusherehekea fainali za kombe la Dunia ambalo kusema kweli ndilo kielelezo cha juu kabisa cha ubora wa soka duniani.
Katika vimbwanga jamaa anavuta sigara akiitafuna bila kuimeza huku akinywa soda ile hali ikiendelea kuwaka.
Ikiwa na moto wake anaitafuna.
Nakuimumunya akisindikizia soda ...agudu agudu....!!!
Kisha anaitoa ikiwa bado na moto na kuendelea kuivuta.. NB Usijaribu (Sigara ni Hatari kwa afya yako)
Coca Cola imekuwa ikiunga mkono mashindano ya soka kwa vijana wadogo chini ya umri wa miaka 15 ya Copa Coca Cola ambayo yanafanyika katika nchi mbalimbali duniani, Tanzania ikiwa ni moja ya nchi hizo.
Licha ya kujishindia zawadi zilizoainishwa wapenzi wa soka kanda ya ziwa watapata fursa ya kushuhudia fainali hizo laivu kwenye vituo mbalimbali katika mikoa hiyo kupitia televisheni zitakazofungwa. Ikiwa ni kuwawezesha Watanzania kuweza kukusanyika pamoja sehemu moja na kuburudika huku wakiangalia mechi za kombe la Dunia.
Picha ya pamoja....wadau wawezeshaji wa shamrashamra za Promosheni ya 'Nunua Kunywa Kusanya na Ushinde'.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.