ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 13, 2014

KWAHERI MZEE MUHDIN NGURUMO.

Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini Tanzania Muhidin Maalim Gurumo aliyekuwa akiitumikia bendi ya Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' amefariki dunia hii leo majira ya saa tisa alasili katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mzee Gurumo amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa kipindi kirefu hali iliyo sababisha astaafu muziki.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Makuburi ambapo shughuli na taratibu zote za mazishi zinafanywa.

Mungu ilaze roho ya marehemu mahali pema  peponi, Amen.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.