Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria. |
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria. |
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja Nigeria |
Tanzania family wakiwa kwenye picha ya pamoja nyumbani kwa balozi, Balozi Ole Njoolay, Abuja Nigeria @ muunganotanzania@50. |
Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania. ikionekana kwa ndani eneo la pool |
Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania @ Muungano Tanzania Inavyoonekana. |
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania |
Asia Idarous & Salma wakiwa kwenye pozi Mwishoni |
ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA
Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni
mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho kubwa la mavazi
ya ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya
Kimataifa ya Nyota tano ya Sheraton Abuja, usiku wa April 25,
huku liki hudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa
kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha Tanzania, nchini humo
Balozi Daniel Ole Njoolay.
Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja,
Nigeria, Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions,
aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum, kwani limeweza kuitangaza
Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
"Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu
Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye
mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja
nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka
ya wamasai kutoka Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia
wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia
mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye
onyesho hilo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy
Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid na wengine wengi. “Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na
kuudumisha ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia
litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje
ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni
wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya
ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija na
hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.