HALMASHAURI ya Jiji la
Mwanza na Manispaa ya Ilemela kushirikiana kwa pamoja kuendesha zoezi la
operesheni safisha Jiji na Manispa ya Ilemela ya kuwaondoa wafanyabiashara
wadogo “machinga na mamalishe” kwenye maeneo wasiyo ruhusiwa kisheria katikati ya mitaa
ya jijini hapa.
Wakizungumza kwa pamoja
juzi katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakurugenzi hao Halfa
Hassan Hida (Jiji la Mwanza) na Zuberi Mbyana (Manispaa ya Ilemela) wameeleza
kuwa uamuzi huo ni utekelezaji wa maagizo ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa na
Kikao cha Ushauri mkoani humo.
Mkurugenzi Hida (Jiji) alieleza kuwa hatua hiyo pia inatokana na
baadhi ya maeneo kuwa na uchafu unaosababishwa na kuwepo kwa wafanyabiashara
wadogo ambao wamekuwa wakifanyabiasha kikolela katika maeneo yasiyoruhusiwa
kisheria ikiwa ni kuvunjwa kwa taratibu na sheria za mipango miji.
“Haiwezekani tukawaacha
watu wafanye biashara kiholela na pengine kwenye maeneo hatarishi, maneo
yasiyoruhusiwa, kandokando ya barabara na wengine kujenga vibanda, viosiki na
kuziba vichochoro ambavyo vinatakiwa kuachwa wazi kwa taratibu na sheria za
mip[ango miji.”alisema
Aidha alieleza kuwa Jiji
limeanza kuutekeleza mpango kabambe wa kuwapanga wafanyabiashara wadogo kwenye
maeneo waliyotengwa na kuruhusiwa kutumiwa na machinga na mamalishe, usafi na
mazingira ili kuweka madhari Mji na Jiji kuwa na mwonekano mzuri wa kupendeza.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mbyana (Manispaa) alisema kwamba lengo la kuungana na Jiji
kutekeleza zoezi hilo linalotarajia kuanza hivi karibuni baada ya kukamilika
taratibu za mwisho kwa kushirikiana na uongozi wa serikali za Wilaya ya
Nyamagana na Ilemela makundi ya machinga, Jiji, Manispaa, Polisi na Mgambo.
“Lengo kuu ni
kuhakikisha wakati wa operesheni hiyo itakapoanza wafanyabiashara hao wasitoke
maeneo ya Jiji na kukimbilia na kuvamia maeneo ya Manispaa kufanyabiashara
kiholela katka sehemu ambazo haturuhusu mtu kufanya shughuli yoyote bila
utaratibu ikiwa ni kuvunja sheria za mipango miji”alisema.
Naye Mwenyekiti wa
Shirika la Umoja wa Wamachinga Mkoa wa Mwanza (SHIUMA) Matondo Masanja, alisema
kwamba wao wanakubaliana na kufanyika operesheni hiyo katika maeneo ambayo
baadhi ya machinga na mamalishe wamevamia bila kufuata utaratibu na
kufanyabiashara kwenye maeneo ambayo hawakuruhusiwa.
“Tulishatengewa maeneo
na kukabidhiwa ili tufanyebiashara kwa uhuru yapatayo 13 ambayo ni Makoroboi, Dampo
soko kuu, Asante moto, uchochoro wa Tanganyika Basi, Libert darajani, Makert,
Nyegezi, Stendi ya zamani ya mwaloni, Rwagasore, Buzuruga, Mirongo, nyuma ya
uwanja wa Nyamagana na Dampo Bandarini” alisisitiza.
Aliongeza kuwa maeneo
mengine ambayo hawaruhusiwi kufanya biashara kiholela ni barabara za Nyerere,
Kenyata, Uwanja wa Ndege, Pamba, Rwagasore, Uhuru, Posta ya zamani, Nkhuruma,
Libert, Karuta, Lumumba, Stesheni-Uhamiaji, Mkuu wa Mkoa, Bantu, Rufiji,
Mkanyenye, Bugando, Mviringo, Mbita, Barewa na zinginezo.
Masanja ametoa wito kwa
wamachinga wote ambao baadhi ni mwanachama wa SHIUMA na makundi mengine kufuata
na kuzingatia kufanyabiashara katika maeneo waliyotengewa badala ya kuzagaa
kila kona na kutandaza chini bidhaa ambapo eneo la Rwagasole bado lipo wazi na
sehemu 530 zimetengwa kwa ajili yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.