ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 29, 2014

ARDHI MABINGWA SAFARI POOL DAR.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Ardhi, Abubakari Hamidu fedha taslimu Shilingi 500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Higher Learning Pool Competition 2014 Mkoa wa Dar es Salaam zilizofanyika katika Ukumbi wa Coco Beach mwishoni mwa wiki.
Ardhi mabingwa Safari Pool Dar.
Na MwandishiWetu.
CHUO cha Ardhi jijini Dar es Salaam kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya mkoa katika mashindano yaliyo shirikishaVyuo vya Elimu ya juu yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika Coco Beach.

Ardhi ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha CBE 13-12, na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na nafasi ya kupeperusha bendera ya jiji la Dar es Salaam katika fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mai 3 na 4,2014 mkoani Kilimanjaro.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na CBE ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=,nafasi ya tatu ni Chuo UDS Mambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/= nanafasi ya nne ni Chuo cha DUCE ambacho kilizawadi wa fedha taslimu Shilingi 100,000/=
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Steven Richard kutoka Chuo cha CBE alitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= pamoja na tiketi ya kuwalikisha mkoa wa Mwanza na mshindi wa pili ni Haji Hussein kutoka chuo cha IFM ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=.

Upande wa wakinadada, JaclineMoleli kutoka Chuo cha TIA alifanikiwa kutwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha wakinadada mkoa kwenye fainali za kitaifa na nafasi ya pili ilichukuliwa na Salma Said kutoka Chuo cha CBE ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shililingi 50,000/=.


Fainali za Kitaifa zitashilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014, Mkoa wa Kilimanjaro.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.