Bugando mabingwa Safari Pool Mwanza.
CHUO cha
Udaktari cha Bugando jijini Mwanza kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya
mchezo wa Pool ngazi ya mkoa katika mashindano ya yaliyoyoshirikisha Vyuo vya
Elimu ya juu yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014”
mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Shooters Pub.
Bugando
ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha CBE 13-10, na hivyo
kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na nafasi ya kupeperusha
bendera ya jiji la Mwanza katika fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika
Mai 3 na 4,2014 mkoani Kilimanjaro.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na CBE ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi
300,000/=,nafasi ya tatu ni Chuo cha St.Agustin(SAUTI) ambao walizawadiwa fedha
taslimu Shilingi 200,000/= na nafasi ya nne ni Chuo cha Kodi(TIA) ambacho
kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja Wanaume,Fredrich Mwangata kutoka Chuo cha SAUTI alitwaa
ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= pamoja na tiketi ya
kuwalikisha mkoa wa Mwanza na mshindi wa pili ni Said Uegen kutoka chuo cha TIA
ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shiling 100,000/=.Upande wa wakinadada, Andressa
Matula kutoka Chuo cha SAUTI alifanikiwa kutwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha
taslimu shilingi 100,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha wakinadada mkoa
kwenye fainali za kitaifa na nafasi ya pili ilichukuliwa na Agnes Jacob kutoka
Chuo cha CBE ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shililingi 50,000/=.
Mkoani Mbeya
chuo kilichofanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa ni Chuo cha Mzumbe ambacho pia
kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 500,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha
jiji la Mbeya katika fainali za kitaifa mkoani Kilimanjaro.Nafasi ya pili
ilichukuliwa na chuo cha MUST ambacho kilizawadiwa Shilingi 300,000/=,nafasi ya
tatu ilichukuliwa na chuo cha TIA ambacho kilizawadiwa Shilingi 200,000/= na
nafasi ya nne ilichukuliwa na chuo cha Tumaini ambacho kilizawadiwa fedha
taslimu Shilingi 100,000/=.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume, Steven Kyasi kutoka chuo cha Mzumbe alitwaa
ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 150,000/= pamoja na nafasi ya
kuwakilisha Mkoa wa Mbeya upande wa wachezaji mmoja mmoja kwenye fainali za
kitaifa Mkoani Kilimanjaro na upande wa wakinadada, Amina Mhina kutoka chuo cha
Mzumbe pia alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu
shilingi 100,000/= pamoja na kuwakilisha jiji la Mbeya upande wa mchezaji mmoja
mmoja katika fainali za kitaifa May 4,2014. Mkoani Kilimanjaro.
Fainali za
Kitaifa zitashilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma,
Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoa
wa Kilimanjaro.
Mabingwa
watetezi wa mashindano hayo ya Pool vyuo yanayodhaminiwa na TBL kupitia Bia
yake ya Safari Lager ni Dar es Salaam, ambacho ni chuo cha CBE.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.