ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 3, 2014

NEW CITY PUB MABINGWA SAFARI NYAMA CHOMA 2014.

Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Dk.Samweli Lazaro (katikati) na jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Nyama Choma, Lawrence Salvi (kulia) wakimkabidhi zawadi ya Kombe na fedha taslimu Shilingi milioni moja (1,000 000) mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 yaliyo fanyika katika Viwanja vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki. Wapili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja wa Tawi la TBL Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula.
Mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi akishangilia na kitita cha Shilingi milioni moja (1,000 000) mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika CCM Ilomba mwishoni mwa wiki .Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashndano hayo, Lawrence Salvi, Meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mbeya, Sameli Lazaro, Meneja wa Tawi la Tbl Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula na Meneja mauzo na matukio Tbl Mbeya, Clauds Chawene.
Mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi akishangilia na kitita cha Shilingi milioni moja (1,000 000) na Kikombe mara baada kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika CCM Ilomba mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashndano hayo, Lawrence Salvi, Meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mbeya, Sameli Lazaro, Meneja wa Tawi la Tbl Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula na Meneja mauzo na matukio TBL Mbeya.
Mashabiki wa New City Pub wakiwa wamembeba juu mpishi mkuu wa pub hiyo, Geofrey Mwashilindi mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.
.Mashabiki wa New City Pub wakiwa wamembeba juu mpishi mkuu wa pub hiyo, Geofrey Mwashilindi mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.
Mashabiki na wapishi wa New City Pub wakishangilia ndani ya gali lao aina ya Pic up yenye namba za usajili T952 BFB wakielekea kwenye Pub yao mara baada ya kuibuka mabingwa wa Safari Nyama Choma 2014 yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.
New City Pub Mabingwa Safari Nyama Choma 2014.
Na Mwandishi Wetu.Mbeya.
New City Pub wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Viwanja vya CCM Ilomba jijini Mbeya na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.

Akizungumza na wakazi Mkoa wa Mbeya waliohudhuria mashindano hayo,Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Dk.Samweli Lazaro aliwashukuru kampuni ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa mbeya kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika jiji la Mbeya.

Alisema Dk.Lazaro kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbali mbali za jijini Mbeya ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia  hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo na sisi kama Serikali tuko pamoja nanyi.

Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mbeya na mwisho aliwapongeza mabingwa wa New City Pub kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2015.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2014, New City Pub na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mbeya waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia naji anatwaa ubingwa.

Mwisho shelukindo aliwaomba wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashndano yajayo ya 2015.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.