ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 3, 2014

WAZIRI SIMBA: WANAWAKE WASOMI VYUO VIKUU MJITAMBUE, PAMBANENI NA MSIKATE TAMAA.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Sophia Simba ambaye pia ni Waziri wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto akifungua na kuzungumza wakati Kongamano la Maendeleo ya Mwanamke miaka 52 ya Uhuru kwenye ukumbi wa Masister wa Kanisa Katoliki Malimbe Nyegezi Jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza Bi. Hellen Bughoe akizungumza na wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Vingine vilivyopo Jijini Mwanza kabla wa Kumkaribisha Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Sophia Simba ambaye ni Waziri wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto

Mgeni rasmi Bi Sophia Simba (Mwenyekiti Taifa) kushoto na Kulia ni Hellen Boghoe (Mwenyekiti Mkoa) na Mwenyekiti wa Tawi la Kambarage SAUT wakiongoza wanachama wapya kula kiapo cha uanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania  wa CCM (UWT).

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali Jijini Mwanza waliojiunga na UWT wakila kiapo baada ya kukabidhiwa Kadi za Umoja huo na Mgeni rasmi Bi Simba wakati wa Kongamano kubwa la kujadili Maendeleo ya Mwanamke ndani ya miaka 52 ya Uhuru .

Mgeni rasmi Bi. Sophia Simba (Mwenyekiti UWT Taifa) akimkabidhi Kadi ya UWT mmoja ya wanachama wapya Mwanafunzi msomi wa  Vyuo Vikuu Jijini Mwanza Malimbe Nyegezi.

Zoezi la kuwakabidhi Kadi wanachama wapya likiendelea.

Sehemu ya Umati wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali waliohudhulia Kongamano hilo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu akiwa na Viongozi na Makada wa CCM wakati wa Kongamano hilo.

Lucy Mlula na Editha Paul wakisoma risala ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanachama wa UWT Jijini Mwanza wakati wa Kongamano hilo.

Mgeni rasmi Bi. Sophia Simba Mwenyekiti wa UWT Taifa (katikati), Bi. Joyce Masunga Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (kulia) na Bi. Hellen Boghoe Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza (kushoto) waliokaa wakiwa na baadhi ya viongozi na makada wa umoja wa wanawake baada ya kufunguliwa kongamano.

Wakati wa kupata picha za kumbukumbu na mgeni rasmi.



Na PETER FABIAN.
MWANZA.

VIJANA wasomi wa Vyuo Vikuu Mkoani Mwanza wanachama wa CCM na Jumuiya ya Wanawake (UWT) wamesema kwamba bado tatizo la Ajira ni kikwanzo kikubwa kwa wanavyuo wahitimu na wanaoendelea vyuoni kujiunga na Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na wanachama wa CCM na UWT wasomi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vingine vilivyopo Jijini Mwanza wakati wa risala yao kwa mgeni rasmi wa Kongamano kubwa la kujadili Maendeleo ya Mwanamke ndani ya miaka 52 ya Uhuru mbele ya Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba (Mjumbe wa NEC CCM Taifa) na Waziri wa Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika ukumbi wa Masista wa Kanisa Katoliki Malimbe Nyegezi Jijini hapa.

Wakisoma risala hiyo iliyoandaliwa na wanavyuo vikuu na vingine Mkoani humo walieleza kuwa pamoja baadhi yao kuhitimu na wengine kuendelea na masomo bado hali hii ya ukosefu wa ajira hukatisha tamaa kwa wahitimu na wanavyuo wanaoendelea katika kujiunga na CCM na Jumuiya zake jambo ambalo Chama na Serikali yake inapaswa kuliangalia kwa upana zaidi na kuliwekea mikakati ya kulipunguza ukubwa wake.

Wasomi hao pia walieleza kuwa lengo la kongamano hili ni kupata uelewa juu ya Maendeleo ya Mwanamke ndani ya miaka 52 ya uhuru na kufahamu kwa undani juu ya Historia ya UWT kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujitathimini kwa wasomi wanawake walioko vyuo vikuu na waliohitimu.

Lucy Mlula na Edita Paul wakisoma risala hiyo walieleza kuwa Hali ya kisiasa katika vyuo vikuu na vingine ni nzuri kwa wastani ikilinganishwa na kipindi cha miaka mitatu iliyopita hii ni kutokana na kuimarisha Wanachama wa CCM na Jumuiya za UWT na UVCCM katika vyuo hivi ikiwa ni kuongeza idadi ya wanachama wapya na kuendelea kueneza sera za CCM kwa wanavyuo wenzetu na jamii inayozunguka vyuo hivyo.

“Sisi wanafunzi Vyuo Vikuu Mkoani Mwanza ambao  pia ni wanachama tunayo mikakati mbalimbali ya kuimarisha Chama na Jumuiya na kufanya Midahalo mbalimbali itakayowahusisha wanachama na wasio wanachama kwa lengo la kujifunza na kujua Itikadi, Sera, Ilani na Malengo ya Chama ikiwa ni nguzo mhimu ya kukiimarisha Chama cha Mapinduzi” walieleza katika risala yao.

Wanafunzi wa Vyuo vikuu vyote Mkoani Mwanza hawakusita kumpongeza Mjumbe wa NEC CCM Taifa kutoka Wilaya ya Tarime Christopher Gachuma kama mfadhili mkuu wa Kongamano hilo wafadhili wengine kwa mchango yao ya fedha na ushauri mzuri iliyopelekea kufanikisha shughuli hiyo.

Naye Waziri Simba akizngumza na wanavyuo vikuu na vingine Mkoani humo walio wanachama wa CCM na Jumuiya ya UWT aliwapongeza kwa kutenga muda wao na kuandaa na kushiriki kongamano hilo kwa wanachama wa UWT na CCM jambo ambalo litaongeza chachu kwa wasomi waliopo vyuo vikuu na wahitimu kujiunga na CCM na Jumuiya zake.

“Kwanza niwahase vijana wasomi ambao ni wanawake kwanza mjitambue, pili msome kwa bidii na tatu acheneni na mambo ya wanaume kwani wanaume ‘Noma’ mnapendeza leo kutokana na kuwa wasomi na wanaume watawapenda mkiwa wasomi tu na mwanaume hawawezi kukupendezesha ukiwa si msomi hivyo  ni vyema mkajitambua sasa  na m kuwa wakakamavu na wapambanaji zaidi” alisisitiza.

Mwenyekiti huyo wa Taifa wa UWT aliwaeleza wasomi hao wanawake wanachama wa jumuiya hiyo kuwa zamani mtoto wa kike hakupewa msukumo wa kupata elimu ya juu kwa baadhi ya makabila na wengi wao ilikuwa ni vigumu kufika darasa la nne wakati huo lakini sasa CCM naSerikali yake ikaweka mikakati na kujenga shule za msingi kila Kijiji, Sekondari za Kata, Vyuo vya Ualimu, VETA na Vyuo Vikuu vya serikali na binafsi.

“Mwanza zamani ilikuwa na sekondari tatu tu ambazo niza serikali ambazo ni Ngaza, Bwiru Girls na Boys lakini leo shule lukuki na  zamani nchi zima Vyuo vikuu vilikuwa vitatu tu ambavyo ni Chuo Kikuu Mlimani na Mhimbili (Dar es salaam) na Mzumbe (Morogoro) sasa viko kila kona ya nchi hii vya serikali, mashirika ya dini na watu binafisi hivyo kazi ni mojas tu kwa wanawake kusoma kwa bidii” alisema.

Waziri Simba alisema kuwa ni mwiko kwa mwanamke kukata tamaa ya kusoma na kuchukua Shahada na Sitashahada eti kutokana na tatizo la ajira na badala yake mjitahidi kuhitimu na kufanya vyema katika taaluma mlizosomea na sasa anzeni kuweka mikakati na mipango ya kujiunga na kuanzisha kikundi pindi mnapohitimu tayari mnakuwa na ajira na zaidi ni kuomba serikalini msaada na serikali itawasaidia.

“Wasomi acheni kuchagua kazi jambo la kuchagua kazi ni lazima mtambue kuwa ni kosa kubwa kuchagua kazi na tumieni taaluma zenu kuanzisha vikundi vya kujiajiri na kuanzisha ajira  kwani serikali bado inatambua kuwepo tatizo la ajira lakini imekuwa ikiajiri kulingana na nafasi zinazopatikana kwani si wasomi wote wataajiliwa.

Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma alisema kwamba pamoja na mambo yaliyojitokeza lazima kuwe na Kanuni za kusaidia kuliongoza kwani bila kuwa na Kanuni mambo hayatakwenda zaidi itakuwa ni vurugu tupu kwa kutambua hilo kuundwa kamati za kushughulikia suala hilo na sasa mjadala na hoja ni jinsi gani kuzipitishe katika kufanya maamuzi ya Katiba hiyo kwa miaka hamsini ijayo.

“Lakini napenda kuwahakikishia kuwa wanawake wote bila kujali Itikadi zetu za kisiasa tumeamua kuungana wa vyama vyote vya kisiasa, mashirika , NGOs, Taasisi na Mawaziri na Wabunge kuhakikisha tunatetea vyema hoja ya asilimia 50% kwa 50 % ili mwanamke ashiriki katika uongozi na kutoa maamuzi” alisisitiza.

Wito wangu kwenu wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu na vingine msikubali kudanganywa na baadhi ya watu na wanasiasa kuwatumieni kuwaunga mkono katika kulisambaratisha Taifa letu hili kwa uchu na tamaa za madaraka kwani wengi wao ni wabinafisi na wenye lengo la kutawala kwa kusema uongo na kuwataka ninyi muwaunge mkono ili wafikie malengo yao hivyo kataaeni kutumika kwa hili.

Kongamano hilo lilihusisha wanavyuo zaid 600 kutoka matawi ya Vyuo Vikuu vya St. Agustine (SAUT) Malimbe cha Nyegezi , Sokoine CBE, Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya na Tiba Cha Katoliki(CUHAS) Bugando, Mipingo, VETA vya Ufundi , UALIMU  Butimba, KILIMO cha Ukiriguru, MIFUGO Cha Mabuki, UVUVI cha Nyegezi na vingine vyenye matawi yake Jijini Mwanza na vilivyopo Mkoani Mwanza.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.