ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 11, 2014

WACHOMA NYAMA MKOA WA MBEYA WAPIGWA DARASA NA TBL.


Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Uchomaji Nyama Bora ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Uchomaji Nyama Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza jaji Mkuu ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama choma. Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Uchomaji Nyama Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza jaji Mkuu ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama choma. Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Picha ya pamoja ya wachoma nyama mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo ya kuchoma nyama yaliyofanyika Airport Pub mkoani Mbeya jana.
Na Mwandishi Wetu. Mbeya
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo kwa  wachoma nyama kutoka Baa mbali mbali za Mkoa wa Mbeya ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Mbeya na Rukwa, Cloud Chawene, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma ukizingatia uchomaji nyama ni moja  sehemu ya kujiingizia kipato katika Bar.

Claudi alisema kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 42 ambao wametunukiwa vyeti vya ushiriki  pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10 watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika semina hiyo.

Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 3, Mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.

Alisema namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.

Aliongeza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika katika Mkoa wa Mbeya itaendelea katika Mikoa mingine ambayo ni Mwanza, Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo vinara wa uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari Lager tofauti na maeneo mengine.

Jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Nyama Choma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Uchomaji Nyama Bora ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.Semina hiyo ilifanyika Airport Pub Mkoani Mbeya jana.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence  Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL wamefikiria jambo la msingi sana lenye mannufaa kwa waandaaji yaani wachoma nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.