ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 11, 2014

WAFANYABIASHARA MWANZA WAGOMA TENA.

Mgomo wa wafanyabiashara umejitokeza tena leo ikiwa ni mara ya pili jijini Mwanza.
Siyo mitaa ya Liberty kunakojaa pilika pilika za biashara, siyo barabara ya Uhuru, Rwagasore, Lumumba wala Kenyata maduka maeneo yote yamefungwa hakuna biashara. SIKILIZA SAUTI ZA WAFANYABIASHARA NA WATEJA KWA KUBOFYA PLAY HAPA CHINI.


Wadau mbalimbali wameonekana wakisota leo kuzisaka huduma na wasifanikiwe kuzipata.
Wafanyabiashara wengine waliamua kwenda kupumzika kabisa majumbani mwao lakini wengine wakiwa pamoja na wafanyakazi wao wameonekana wakiketi nje ya maduka yao kusikilizia pengine kutakuwa na mabadiliko huku hasara ikiwasubiri.
Huduma za vyakula, pembejeo kote hazikupatikana kwa siku ya leo.
Hali tete kwa biashara bidhaa zote.
Mitaa hii huwa na purukushani nyingi za hapa na pale lakini leo kweupeeee....
Mtaa huu unao unga barabara za Lumumba, mitaa ya Shinyanga Hotel huwa na pilika za haja lakini leo pakavu mithili ya uwanja wa kandanda.
Ni wauza vocha na vyakula vidogo vidogo ndio wamebakia ingawa nao wanalalama kuwa hakuna wateja.
vichochoro vya maduka nako hola..
Ni saa tisa alasili lakini hali ni tete hakuna huduma.
Kufuatia mgomo huo athari kubwa  zimeonekana kwa sekta mbalimbali za huduma nyiginezo kudorora, kuanzia wadau wa vyombo vya usafiri kama daladala na tax ambao hutegemea pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi kufanya huduma ya usafiri, hivyo kwa siku ya leo kipato chao kimeshuka kwa kiwango kikubwa.
Hapa napo leo ni pakavu.
Spea za magari, vifaa vya ujenzi, bidhaa za simu zimeadimika hii leo.
Mtaa wa msikiti wa ijumaa jijini Mwanza.
Mtaa wa Nyerere jijini Mwanza.
Mitaa ya barabara ya posta to Mwanza Hotel maduka yote ya wafanya biashra yalikuwa yamepigwa makufuli kufuatia mgomo huo ambao bado haijajulikana kuwa utakoma lini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.