ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 11, 2014

CHEMICOTEX YAJA NA BIDHAA YA TRESSA KUBORESHA UREMBO WA NYWELE ZA MTANZANIA.

Baadhi ya wanamitindo wakionyesha umahili wao wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.


Msanii wa nyimbo za kizazi kipya, Elias Barnabas akiimba huku akipiga gitaa wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa.Uziduzi ulifanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Bendi ya Machozi, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’(kushoto) akiimba sambamba na waimbaji wake wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Meneja wa bidhaa za TreSSa, Dorith Godfrey(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Balozi wa bidhaa za TreSSa, Elgiver Godwin(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Meneja masoko wa bidhaa za TreSSa, Manoj Kumar (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
 TAARIFA KWA VYOMBO
Toleo la Leo
Chemicotex yaja na bidhaa ya Tressa kuboresha urembo wa nywele za Mtanzania.
Dar es Salaam, Februari 10,2014:Kampuni ya Chemicotex nchini Tanzania leo imezindua bidhaa mpya ya  vipodozi vya nywele aina ya Tressa iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kuboresha urembo wa nywele za Mwanamke wa Kitanzania.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wamiliki wa Saluni,wanamuziki na wanamitindo mbalimbali.

Tressa Professionals ni ubunifu kwenye tasnia ya utunzaji nywele, ikiwa na mchanganyiko wa kipeke wa sayansi na asili. Bidhaa sa TreSSa zina viungo kama vile; Parachichi, Mafuta ya Jojoba, Indian Hemp na protini za nyewele kama vile Keratin.

Bidhaa hizi vimefanyiwa uchunguzi na kujaribiwa kwenye nywele za Kitanzania na kumpa Uhuru mwanamke wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla kutokatika kwa nywele zake. Sasa mwanamke ana uhuru wa kuchangua bidhaa inayoendana na mtindo wa nywele aupendao.
TreSSa ina bidhaa mbalimbali za vipodozi vya nywele zikiwemo; Relaxers (aina ya regular na super), Neutralising plus Strengthening Shampoo inayoweza kutumika kila siku, Hair Food (iliyo na mafuta ya Jojoba na Indian Hemp) inayong’arisha na kupooza nyewele na ngozi ya kichwa, Moisturising Pink Lotion kwa matumizi ya kila siku naHair Mayonnaise iliyo na protini kwa nywele zenye afya.

Akiongea na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Chemicotex, BwanaAbhijit Sanyal, alisema, “Kampuni ya Chemicotex imekuwa mstari wa mbele kuleta bidhaa zenye ubora kwa watu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. TreSSa ni mfano wa ahadi endelevu wa ahadi zetu wa kutowa bidhaa zenye thamani kubwa kwa watu wa Tanzania”.

Tressa Professionals ni bidhaa iliyo tengenezwa na kampuni ya Chemicotex, amabao ni watengenezaji wa maarufu kama dawa ya meno ya Whitedent na Bannister’s Glycerine.

Afisa  Mkuu wa Masoko, Chemicotex, Bwana Ranendra Ojha, alisitiza,  “Utafiti umetuonyesha kwamba utunzaji wa nywele ni jambo la muhimu kwa wanawake wa Kitanzania. Hatimaye TreSSa imewapa Uhuru wanawake wa kutokatika kwa nywele zao, ambalo ni tatizo kwa wanawake wakati wakitengeneza nywele.”

Tuna mipango ya kuwafikia wanawake wote nchini kupitia semina, warsha, vipindi vya tv na ushirikiano wetu na saluni ili kuhakikisha mwanamke anapte fursa ya kutengeneza mitindo ya nywele aipendayo kwa kutumia TreSSa.” Bwana Ojha aliongezea alipokuwa akizungumzia mipango ya TreSSa.

Kampuni hii ina mipango madhubuti ya kimasoko na kuitangaza bidhaa ya TreSSa, aidha kampuni ina malengo ya kuzoa asilimia 25 ya soko la utunzaji nywele ndani ya miaka 3.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.