ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 5, 2014

BancABC YATOA MSAADA WA PIKIPIKI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUTOKOMEZA UHALIFU.

Meneja  wa Tawi la BancABC Mkoa wa Arusha, Anna Kavishe(kushoto) akimkabidhi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, funguo za Pikipiki  aina ya Boxer yenye thamani ya Shilingi milioni nne(4,000 000/=)  ikiwa ni msaada wa kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi mkoani humo za kutokomeza uhalifu.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Meneja  wa Tawi la BancABC Mkoa wa Arusha, Anna Kavishe, akimkabidhi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, funguo za Pikipiki  aina ya Boxer yenye thamani ya Shilingi milioni nne(4,000 000/=)  ikiwa ni msaada wa kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi mkoani humo za kutokomeza uhalifu.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Meneja  wa Tawi la BancABC Mkoa wa Arusha, Anna Kavishe(wa tatu kushoto) akimvisha kofia aina ya Helemeti, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, mara baada ya kumkabidhi  funguo za Pikipiki  aina ya Boxer yenye thamani ya Shilingi milioni nne(4,000 000/=)  ikiwa ni msaada wa kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi mkoani humo za kutokomeza uhalifu.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, akijaribu kuendesha pikipiki aina ya Boxer mara baada ya kukabidhiwa na Meneja  wa Tawi la BancABC Mkoa wa Arusha, Anna Kavishe(kushoto) yenye thamani ya Shilingi milioni nne(4,000 000/=)  ikiwa ni msaada wa kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi mkoani humo za kutokomeza uhalifu.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Na Mwandishi Wetu.Arusha
MENEJA wa Tawi la BancABC Arusha, Anna Kavishe amekabidhi msaada wa pikipiki zenye thamani ya milioni nne(4,000 000/=) kwa Kamada wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha,  Liberatus Sabas, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono zoezi la kupunguza uhalifu mkoani hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo Meneja wa Tawi la BancABC Mkoa wa Arusha, Anna Kavishe alisema jukumu la ulinzi ni la kila mtu hivyo wao kamaa Benki wanatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia na mali zao ndio maana wameshawishika kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi katika Mkoa wa Arusha kwa kuhakikisha wakazi wa Arusha wanakuwa salama pamoja na mali zao.
Kavishe pia alitoa wito kwa Makampuni na Taasisi zingine za kibiashara kuiga mfano waliounyesha BancABC kulion ga mkono jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha katika harakati za kuimarisha ulinzi na Usalama ili jiji la Arusha liwe mfano kwa mikoa mingine kwa utulivu na amani kwani bila amani na utulivu hakuna Biashara na bila biashara hakuna maendeleo.
Tawi BancABC Mkoa wa Arusha ni mwaka wa tatu sasa tangu lianze kutoa huduma zake za kibenki kwa Mkoa huo na jamii ya wakazi wa Arusha wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma nzuri zinazotolewa na benki hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.