ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 5, 2014

UINGEREZA YASAINI HATI YA MAKUBALIANO NA UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO.

 Kaimu mkurugenzi wa UTPC Victor Maleko (kushoto) akipokea hati ya makubaliano toka kwa Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Evidence for Action Craig Ferla lenye makao yake makuu nchini Uingereza ili kukuza uwajibikaji wa wanahabari katika uwasilishaji taarifa katika jamii kulinda afya ya Mama, Mzazi na Mtoto kwa lengo la kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ujauzito.
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la (Evidence for Action)  lenye makao yake makuu nchini Uingereza leo limesaini hati ya makubaliano na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) ili kukuza uwajibikaji katika kulinda afya ya Mama, Mzazi na Mtoto kwa lengo la kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ujauzito.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya Duniani (WHO) akina mama wajawaziti 8500 pamoja na watoto wachanga 50,000 hufariki Dunia kila mwaka kutokana na vifo vitokanavyo na ujauzito vinavosababishwa na ukosefu wa huduma bora za afya hususani kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni.
Kaimu mkurugenzi wa UTPC Victor Maleko, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza mara baada ya makubaliano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari ziliopo mtaa wa Isamilo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza Kaimu mkurugenzi wa (UTPC) Victor Maleko amesema makubaliano hayo yanalenga kuwajenga wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia huduma ya afya.
Craig Ferla.
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Evidence for Action Craig Ferla amesema shirika hilo limefanya makubaliano hayo ili kuwawezesha waandishi wa habari kutoa taarifa za kina kuhusu njia sahihi za kulinda afya ya Mama, Mzazi na Mtoto kwa lengo la kuwawezesha wadau wengine kufahamu njia sahihi za kujilinda ili kuepuka vifo hivyo.
Makubaliano ya mkataba huo wa kukuza uwajibikaji katika kulinda afya ya Mama, Mazi na Mtoto yanatarajiwa kutekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne katika mikoa yote nchini Tanzania.
Rais wa UTPC Keneth Sembaya akitoa ufafanuzi ni namna gani mafunzo hayo yatakavyo kuza weredi wa waandishi wa habari.
Taswira ya meza kuu na engo moja wapo ya kusanyiko la makubaliano.
Wadau wa habari.
Kutoka kushoto mbele ni David Azaria na Sita Tuma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.