Airtel kuboresha mitambo ya huduma ya Airtel money mwishoni mwa wiki hii
· Mabadiliko yataleta ufanisi kwa huduma ya Airtel money
· Mabadiliko yatawezesha wateja kufanya mambo mengi na kuongeza watumiaji wa huduma ya Airtel money
· Mabadiliko yataongeza matumizi ya huduma ya Airtel money Tanzania
Dar es Salam Februri 7 2014: Airtel Tanzania, kampuni inayoongoza kwa kutoa
huduma za kibunifu na zenye ubora nchini iko katika mchakato wa kuboresha
mitambo ya huduma ya Airtel money na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.
Mabadiliko haya yatafanyika mwishoni mwa wiki hii tarehe 7 hadi 9 februari 2014
ambapo baada ya maboresho hayo wateja wa Airtel Money watafurahia ufanisi bora
wa mtambo wa Airtel money wakati wowote watakapotaka kufanya malipo
mbalimbali kwa kupitia huduma za kifedha za simu za mkononi
Maboresho hayo ya mitambo ya Airtel money wateja wataweza
kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuunganishwa na huduma mbalimbali
na kuongeza ufanisi zaidi . Huduma hii itawawezesha wateja kununua muda wa
maongezi, kutuma pesa, na kufanya malipo ya huduma mbalimbali, kutoa na kutuma
pesa pamoja na kuongeza huduma mbalimbali wanazotakana kuzitumia kupitia
Menu/orodha ya mpya ya huduma hiyo ya Airtel Money zikiwemo zile za
kuunganishwa na huduma za kibenki
Akiongea kuhusu mabadiliko hayo ya mitambo, Mkurugenzi wa
kitengo cha Mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kuboreshwa kwa mitambo
yetu ya huduma za kifedha ya Airtel money ni sehemu ya malengo ya Airtel
ya kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala ya pesa mahali popote wakati wowote
kwa urahisi zaidi. Tunaamini maboresho haya yataleta urahisi zaidi kwa
watumiaji wa huduma ya Airtel money nchini”
Bi Singano aliendelea kusema, “wakati wa kuboresha hatutegemei
kuwa na matatizo yoyote wakati wa zoezi hilo la kuborehsha mitambo yetu na
tunawaomba wateja wetu wawe wavumilivu kwa usumbufu utakaojitokeza wakati
tutakapokuwa tunafanya zoezi hili kuanzia jumamosi saa 3 usiku hadi jumapili
asubuhi . tunawahakikishia wateja wetu wa Airtel Money wote kuwa tunafanya
mabadiliko yatakayoleta ufanisi zaidi kwa watumiaji wote, mashirika
binafsi, serikali, mabenki na wadau mbalimbali. Huduma yetu kwa wateja
inapatikana masaaa 24 siku zote 7 za wiki ili kuweza kutoa huduma iwapo
kutakuwa na matatizo yoyote. Pia tutaweza kuwasaidia wateja wetu
watakaowasilisha baadhi ya matatizo kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii
yaani Facebook and Twitter.”
Maboresho ya Airtel Money yenye lengo la kuendelea kutoa huduma
Bora zaidi pia yanadhihirisha jitihada za Airtel kuendeleza ubunifu wa hali ya
juu kwa kuleta teknolojia mpya za kisasa zaidi katika sekta ya
mawasiliano nchini Tanzania, Tumedhamiria kuwaletea wateja wetu huduma bora
zaidi inayokwenda sambamba na mahitaji yao ya kila siku. Hii ndio sababu kubwa
inayotufanya Airtel kuboresha mtambo wetu wa huduma hii ya Airtel Money kuwa wa
kisasa zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.