ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 7, 2014

FAINALI ZA LAKAIRO CUP 2014 ZILIVYONAKSHI MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM JIMBO LA RORYA .

Mgeni rasmi wa michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa CCM mkoa mpya wa Geita Joseph Msukuma akiiongoza meza kuu katika zoezi la kusalimiana na wachezaji wa timu ya Alonga Fc pamoja na Nyabikondo Fc katika mchezo wa awali wa kusaka mshindi nafasi ya tatu wa michuano hiyo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kogalo Utegi wilayani Rorya mkoani Mara ambapo hadi mwisho Alonga Fc walinyuka Nyabikondo Fc bao 2-1 na kutawazwa washindi wa tatu.
Muasisi wa michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM), Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Nyabikondo Fc katika mchezo wa awali wa kusaka mshindi nafasi ya tatu wa michuano hiyo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kogalo Utegi wilayani Rorya mkoani Mara ambapo hadi mwisho Alonga Fc walinyuka Nyabikondo Fc bao 2-1 na kutawazwa washindi wa tatu.
Katika zoezi la kusalimiana kwa wachezaji wa timu ya Alonga Fc pamoja na Nyabikondo Fc hawakushikana kabisa mikono zaidi ya wachezaji wa timu hizo kupigiana makofi.
Alonga Fc .
Nyabikondo Fc.
Mtanange kati ya Alonga Fc pamoja na Nyabikondo Fc ukaanza ikiwa ni mchezo wa awali wa kusaka mshindi nafasi ya tatu wa michuano hiyo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kogalo Utegi wilayani Rorya mkoani Mara ambapo hadi mwisho Alonga Fc walinyuka Nyabikondo Fc bao 2-1 na kutawazwa washindi wa tatu wakijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili.
Soka linavyo vuta hisia.
Hatari toka winga ya kushoto kuelekea katika lango la Nyabikondo Fc iliyozaa bao la pili na la ushindi kwa Alonga Fc.
Mashabiki na kibwengo chao walichokivisha magwanda na juu kikavalishwa skafu ya kijani ya CCM na kitambaa cha njano rangi kikiandikwa 'KARIBUNI CCM'.
Ummati ulifurika katika michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa CCM mkoa mpya wa Geita uliendelea kuongezeka kadri muda ulivokuwa ukisonga mbele kwani mkutano na hotuba fupi ya Maadhimisho ilifuata mara baada ya michezo kumalizika.
Kibendera cha CCM ndipo ilipokuwa engo ya kona na kibendera cha Mountain Dew ndiyo uzio kwa mashabiki ambapo Pepsi walikuwa ni moja ya wadhamini wa Michuano ya Lakairo Cup 2014.
Watu wa kada mbalimbali wameshiriki Maadhimisho haya ya Miaka 37 ya CCM jimbo la Rorya mkoani Mara.
Wananchi wamekuja navyombo vyao vya usafiri.
Kwa utulivuu matukio yakiendelea.
Engo moja wapo ya jukwaa walilokaa makada na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rorya wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakijiri katika uwanja wa Kogalo Utegi wilayani humo mkoani Mara.
Hapa niliombwa na wadau niwachukue picha wakisema nao wanataka kuonekana mtandaoni kuwa liibuka kwenye tukio.
Huu ulikuwa mchezo wa awali kumsaka mshindi wa tatu michuano la Lakairo Cup na Maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kaa tayari kushuhudia 'part two' ambayo itajumuisha mchezo wa fainali kati ya Utegi Fc na Nyanduga Fc.

Michuano ya Lakairo Cup 2014 ilishirikisha jumla ya timu 140, ikifanyika ndani ya miezi mitatu ikwa na malengo ya kuwafanya vijana kuwa bize na shughuli za kufanya ili kuwaondoa vijiweni sambamba na kuwaepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na uzinzi hatua ambazo kwa kiwango kikubwa zimefanikiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.