ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 18, 2013

MAASKOFU ,WACHUNGANJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA

 Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste mkoani Mwanza Alexanda Mwakisumbwa (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. wengine katika picha ni Mwenyekiti msaidizi Zenobius Isaya ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Filadelfia Church (kushoto) na Mwenyekiti wa Makanisa ya Kiprotestant Askofu Charles Sekelwa (kulia).







MAASKOFU ,WACHUNGANJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA 

MAASKOFU na Wachungaji wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza,wameunga mkono Tamasha la Muziki wa Injili, baada ya kuridhia Kwaya ya Makanisa yao kushiriki tamasha hilo.

Tamasha hilo la Krismasi la  Muziki wa Injili, litafanyika Desemba 25 mwaka huu,majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha pamoja kati yao na waandaaji wa tamasha hilo, The Great Lake  Zone Entertainment,kilichofanyika Vizano hoteli, Maaskofu hao walisema, mbali na kutangaza neno la Mungu na utukufu wake, litasaidaia kuutangaza muziki wa injili wa kwaya za Makanisa hayo ya Jijini hapa.

“Ni maono mazuri kwa waandaaji wa tamasha hilo,na sisi Maaskofu tunapaswa kuwaunga mkono badala ya kuwakatisha tamaa.Haiwezekani tukatafute waimbaji kuoka Dar es salaam badala ya kutumia hawa tulionao hapa,”alisema 

Askofu wa Kanisa la Menonite Tanzania (KMT) Nyakato,Albert Randa, alisema teknolojia imepanuka tofauti na zamani ambapo nyimbo nyingi na nzuri za kwaya hazikupata fursa ya kurekodiwa.Kwamba ukanda wa Ziwa hasa Mwanza na Mara kuna waimbaji wazuri wenye vipaji.

Askofu Charles Sekelwa,alisema jambo hilo (tamasha) likienda vizuri, ni heshima kwa waandaaji na akawataka Maaskofu wasiwe sehemu ya ubaya bali uzuri ili sifa na utukufu zimwendee Mungu ikiwa ni pamoja na kuwahamsisha waumini wao kuja kushiriki tamasha hilo ili kuwaepusha na starehe zinazomchukiza Mungu. 

Hata hivyo Askofu Sekelwa ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja huo wa Makanisa ya Kikristo Mwanza,  alionya tamasha hilo lisiwe la kisiasa ndani yake, ili kuepusha maaskofu kuchafuliwa kutokana na kuunga kwao mkono na ushiriki wao.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel,mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, na kutakuwa na chakula cha usiku katika hoteli ya Malaika baada ya tamasha hilo. 

Tamasha hilo la muziki wa Injili litafanyika uwanja wa CCM Kirumba kuadhimisha kuzaliwa kwa Masiha (Yesu) kiingilio kitakuwa shilingi 2000 kwa watu wazima ambapo watoto watalipa shilingi 1000.

Tayari wasanii na waimbaji maarufu, Martha Mwaipaja ,Nesta Sanga, Neema Nga’sha,Daniel Safari na mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) Pascal Cassian,watanogesha tamasha hilo kwa vibao vyao vilivyotamba na vinavyotamba kwa sasa katika muziki wa Injili,wamethibitisha kushiriki.

Wengine watakaopaza sauti zao siku hiyo ni Seiri Andrew (Nzega Tabora), Joseph Vedasto (Geita), Dan Sanga na Mary Msigwa (Iringa), Pendo Kanyumi, Christine Victor, Betty Lucas, Excellence Band, Revival Mission Band na kwaya mbalimbali kutoka Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.