ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 18, 2013

REMMY WILLIAMS ATUA NCHINI.

MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Will akiwasili nchini akitokea Italy.


MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Will  (kushoto ) akiwasili nchini akitokea Italy kulia ni meneja wake nchini Italy Wactor Fizio walipowasili nchini Tanzania.


MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams


MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams katikati akilakiwa na baadhi ya warembo waliojitokeza kumpokea msanii huyo.


MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams akiwa ameshikwa mkono na meneja wake wa Tanzania Mcdennis Mgatha.
Na Mwandishi Wetu

MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams anaefanya shughuli za mziki nchini Ital ameingia nchini jana na kutua jijni Dar es salaam kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii wenzake nchini.

Akizungumzia ujio wake mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu julius nyerere Dar es salaam anasema kuwa nawapenda wasanii wote wa Tanzania anavyofanya vema nchini na kazi zao nyingi zinavuka mipaka kwa ajili ya kujitangaza kimataifa.


Hata hivyo yeye amejitokeza kuupaisha mziki huo kwa kushirikiana na wasanii watakao chaguliwa kushirikiana nae.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo meneja wake nchini Mcdennis Mgatha amesema msanii huyo kaja nchini kwa ajili ya kufanya colab na wasanii hapa nchini hivyo wapenzi wa mziki wakae mkao wa kula kwani ana vitu vingi sana alivyo waandalia ikiwemo nyimbo mpya pamoja na kufanya shoo kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hizo. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.