TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
TANZANIA
DISTILLERIES LIMITED(TDL) YAZINDUA
PROMOSHENI YASHINDANO LA KUMSAKA MSHINDI ATAKAE PATA FURSA YA KWENDA KUTEMBELEA
SHAMBA KUTENGENEZA KINYWAJI CHA AMARULA NCHINI AFRIKA KUSINI LIJULIKANALO KAMA
“AMARULA PAN AFRICAPROMOTION”.
Dar es Salaam,Jumanne 17 Disemba 2013:
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) leo
imetangaza promosheni ya shindano la kumsaka mshindi wa anayetumia kinywaji cha
Amarula, kinacho tengenezwa nchini Afrika Kusini na kusambazwa na TDL nchini
maarufu kama nyumba ya Konyagi katika promosheni iliyozinduliwa leo Shoprite
Mlimani City jijini Dar es Salam ijulikanayo kama “Amarula Pan Africa Promotion”.
Akizungumza na waandishi
wa habari, Meneja Bidhaa wa TDL, Diana Baliagati alisema shindano hili la
kumsaka mtumiaji wa Amarula litaanza rasmiDesemba 16,2013 hadi Januari 14, 2014.
Diana alisema lengo hasa
ikiwa ni kuwapa fursa wanywaji wa Amarula kwenda kutembelea nchi ya Afrika Kusini
na kushuhudua shamba la Amarula na kujionea matunda ambayo hutumika
kutengenezea kinywaji cha Amarula.
Mshindi katika shindano
hili,atapata tiketi moja itakayomuwezesha kusafari na mwenzake kwa ajili ya
kwenda kushuhudia shamba la AMARULA,nchini Afrika Kusini na kufikia katika
Hoteli ya nyota tano(5Star), alisema Diana.
Meneja bidhaa wa TDL,
Diana Baliagati alisema, ili kupata nafasi ya kujishindia tiketi,mshiriki
anapashwa kujaza kuponi zilizo katika shingo ya chupa kubwa za Amarula
zinazouzwa katika maduka makubwa yote ya Shopritehusika.Chupa hizo za shindano
la Amarula Pan Africa Promotion zitakuwa
zikipatika kwenye maduka ya Shoprite tu.
Mshindi wa Amarula Pan Africa Promotion
atapatikana kupitia drooitakayofanyika
Januari 14,2014, na safari itakuwa mwezi Februari.Mshindi atapewa taarifa zote
zinazohusika na safarihiyo mara baada ya droo kufanyika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.