ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 11, 2013

ZIARA YA RAIS GEITA: WAANDISHI NA MENEJA WA MSD WAPATA AJALI

Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
Askari akilikagua gari.
Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita.
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
GEITA: Meneja wa Boharia ya Dawa (MSD) Kanda ya Ziwa pamoja na waandishi watatu wa habari wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakitumia katika msafara Rais  Jakaya Kikwete mkoani Geita kupinduka.
Ajali hiyo imetokea leo eneo la Nyankumbu kata ya Kalangalala, majira ya saa 3:54 asubuhi, wakati gari aina ya Toyota Land Cruiser, lilipopinduka muda mfupi wakati msafara wa Rais Kikwete ulipoanza safari kuelekea wilayani Nyang’wale kwa ziara.
Walionusurika katika ajali hiyo ni mwandishi Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa www.mabadiliko.com, Peter Makunga wa Radio Free Afrika, meneja wa MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Meneja Tabura alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi wa Lami iliyokuwa umewekwa juu ya tuta la Barabara ya moramu inayoendelea kujengwa, hali iliyosababisha gari hili kupoteza mwelekeo na kuacha njia na kupinduka.
“Hii barabara ambayo msafara unapita ipo katika matengenezo, inawekewa Lami, inaonekana wakandarasi hawa waliamua kumwaga lami rojo ili kwa ajili ya kuja kuweka kokoto, hivyo barabara ilikuwa ikiteleza, ndicho chanzo cha ajali yetu,” alieleza Tabura.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Geita, Dk. Adam Sijaona alieleza kuwa wahanga wa ajali hao walipokelewa Hospitalini hapo na kuchunguzwa afya zao, wanne kati yao waliruhusiwa kuendelea na shughuli zao, lakini mmoja tuliamua kumpumzisha kwa muda kutokana na kuwa na maumivu makali ya mkono wa kulia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.