ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 20, 2013

CRDB YATUMIA MILIONI 50 KUKARABATI WARD YA WAJAWAZITO HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria ufunguzi ward ya wajawazito katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza ambapo CRDB iliifunga kwa muda ward hiyo ilikuifanyia ukarabati madhubuti na kuwa ya kisasa zaidi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza, Mkurugenzi wa BMC Prof. Charles Majinge, Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dr. Charles Kimei (aliyenyanyua mkono), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na mmoja kati ya maafisa wa CRDB. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akifungua pazia la bango la wadhamini katika hafla ya kukabidhi ward ya wajawazito Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza iliyokarabatiwa na CRDB Benki. 
Pia CRDB imekabidhi mablanketi, vyandarua, vitanda na mashuka pamoja na mapazia ya kusitiri huduma maalum kwa ward ya wajawazito Bugando.
Huduma ya Afya ya mama na mtoto inakabiliwa na changamoto nyingi sana moja wapo ni ugonjwa wa malaria ambao umekuwa moja ya vyanzo vikuu vya vifo vya watoto nchini, kwa kuliona hilo CRDB wamehakikisha kila kitanda kina neti yenye ukubwa wa kutosha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu akishiriki utandikaji mashuka na blanketi katika ward ya wajawazito Hospitali ya Rufaa Bugando iliyokarabatiwa na CRDB Bank.
Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Bugando wakitandika 'kiprofesheno' zaidi...
Idadi ya wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na kuhudumiwa na wataalamu wenye  ujuzi imeongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2011 na kufikia asilimia 65 mwaka 2013, hivyo mchango huu wa CRDB Bank unaihamasisha jamii kukimbilia kwenye vituo vya afya kwani kuna uhakika wa kupata huduma bora zaidi.
'Kiprofesheno' zaidi..!!
Ukarabati huu umegusa kila engo hadi hapa (sekta nyeti)
Mchango wa magodoro, vitanda, matandiko, neti pamoja na mapazia ya kusitiri kwa huduma za dharura ni kazi nzuri iliyofanywa na CRDB kwa vyumba vyote vya ward ya wajawazito Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Chumba kingine katika ward hiyo ya wajawazito BMC.
Furaha.
Blogger G. Sengo akisaidizana na muuguzi wa ward ya Wajawazito Dr. Asha Juma kutandika mashuka vitanda vya ward hiyo ya Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza iliyokarabatiwa na CRDB Bank.
"Asilimia 35 ya wakazi wa Mwanza huugua maralia kila mwaka, na malaria bado ni ugunjwa tishio kwa mkoa wetu na nchi kwa ujumla, hivyo mchango wenu wa ukarabati na vifaa vyake vikiwemo vyandarua ni kielelezo tosha cha benki ya CRDB kuwakumbusha wananchi juuu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria" kauli ya mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo.
"Tukio hili tunalifanya ikiwa ni hatua za kurejesha kiasi cha fungu la faida kwa jamii, afya ya  jamii inapoimarika ndipo watu wake wanapopata nafasi ya kufanya kazi na kuwekeza kwenye mabenki yetu na hapo ndipo faida inapopatikana"

"Jamii inapokuwa dhoofu kiafya basi kazi nazo haziendi, uwekezaji wa tija unapungua na faida inakosekana, hivyo tumeamua kuwekeza katika kuboresha afya ya jamii ili tuzidi kupata faida" kauli ya Dr. Kimei.
"Mmekuwa mfano, ninaamini sekta nyingine za fedha zitakuja kuwekeza hapa katika hospitali hii ya pili kwa ukubwa nchini yenye kuhudumia watu takribani milioni 18 ya wakazi wa kanda ya ziwa " kauli ya Prof. Majinge.
Mashuhuda na wafanyakazi wa CRDB walio hudhuria hafla hiyo.
Burudani toka Bujora Nyoka Dance.
Wadau haflani.
Kusanyiko haflani.
Shukurani za akina mama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.