ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 20, 2013

JULIUS NYAISANGA KATUTOKA.

Ni Habari zilizotufikia saa chache zilizopita kutoka mkoani Morogoro zinasema Mtangazaji Julius Nyaisanga amefariki Dunia. 

Hakika ni taarifa ya kushtua katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na habari za kifo cha Mtangazaji mkongwe nchini Tanzania, Julius Nyaisanga, aliyekuwa mfanyakazi wa Abood Media mjini Morogoro.

Taarifa kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa redio hiyo ambaye hakupenda jina lake liwekwe hadharani kwani siyo msemaji wa familia wala redio hiyo zimesema kuwa Nyaisanga maarufu kama Uncle J amefariki katika hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro ambako alikuwa akipatiwa matibabu, akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu.

Taarifa zaidi kuwajia kadri zitakavyokuwa zikipatikana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.