WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza(TANROAD) hatimaye imeanza
utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na serikali kwa kuanza mradi
wa ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita
17.8 ili kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo kuingia Jijini
Mwanza.
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonarld Kadashi alisema
serikali baada ya kupata fedha ilitangaza kazi na kupatikana Mkandarasi
aliyeshinda ambaye ni Kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Ltd ya Jijini
Mwanza ambapo kwa sasa Mkandarasi huyo yupo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa
barabara hiyo ya Usagara-Kisesa ya kiwango cha lami.
“Kazi imeanza tangu mwezi Julai mwaka huu na inaendelea kwa
kasi na tayari Mkandarasi aliyopo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara
hiyo anaendelea na kazi ya kusafisha barabara ambapo kilomita 5
tayari na ujenzi wa madaraja sanjari na ujenzi wa nyumba za kambi ya Mhandisi
mushauri na msimamizi na wafanyakazi wake kisha kuendelea na ujenzi wa kuweka
lami”alisema
Mhandisi Kadashi alisema kwamba Rais Kikwete aliomba kufanyika
mchakato wa kuanza ujenzi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa wakati alipokuwa
akifungua barabara ya Usagara-Kigongo kupitia Mjini Sengerema, Geita, Bukoba
hadi Kigoma ya Lami mwaka 2011 na hivyo kuahidi kwa wananchi wa Wilaya za
Misungwi na Magu ujenzi huo kwa kueleza kuwa ni lazima barabara hiyo ijengwe
kwa kiwango cha lami.
“Ujenzi wa barabara hii umeanza mwezi Julai mwaka huu na
unaendelea na utasaidia magari yanayotoka barabara ya Usagara – Geita yenye
urefu wa kilomita 90 na yale ya Kutoka njia ya Shinyanga-Mwanza yakielekea
Mkoani Mara hadi nchi jirani ya Kenya kutolazimika kupitia katikati ya Jiji la
Mwanza kwanza kabla ya kuendelea na safari zao,pia kutoa huduma ya
usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo. alisema Meneja.
Meneja, Kadashi alieleza kwamba mradi huo ulibuniwa na serikali,
awali ulikuwa utekelezwe na Jumuiya ya Ulaya (EU) lakini walijitoa kuufadhili
na kusababisha mradi kuchelewa kuanza kutokana na kukosa fedha na sasa mradi
huu umepata fedha na unatekelezwa na Serikali kwa asilimia mia moja kupitia
Wizara ya Ujenzi ambayo mbali na kugaramia ujenzi pia itawalipa fidia wananchi
kwa kutumia taratibu za ndani wale watakaopitiwa na barabara hiyo.
“Wananchi wa maeneo hayo wasiwe na wasiwasi, serikali itawalipa
fidia wananchi wote walio nje ya hifadhi ya barabara watakaoguswa na kupitiwa
na mradi huo na uthamini unaendelea kwenye maeneo mengine yaliyobaki, lakini
wale waliovamia na kufanya ujenzi ndani ya maeneo ya hifadhi ya barabara hiyo ya
Usagara-Kisesa serikali haita walipa fidia na waanze kubomoa nyumba na vibanda
vyao kwa mujibu wa sheria ili kuruhusu ujenzi wa mradi huo”alisisitiza
Mhandisi Kadashi alisema kwamba ujenzi wa mradi huo utagarimu
shilingi bilioni 17.8 na unataraji kukamilika kwa kipindi cha miezi 15 kuanzia
mwezi Julai mwaka huu ambapo tayari wananchi wameupokea na baadhi yao wameanza
kuvunja nyumba na vibanda vyao baada ya kuwaelimisha kwenye mikutano ya hadhara
na kuitambua sheria inavyoelekeza na viongozi wa vijiji wamekuwa wakitusaidia
kuwaelimisha.
Uchimbaji udongo. |
“Tuwashukuru wananchi kwa kukubali kuupokea mradi huo na
kutuelewa, viongozi wa serikali za vijiji wamekuwa ni msaada mkubwa kwa
wananchi wao na kwa serikali pia hili ni jambo zuri na tuliwasihii sana
wananchi kuacha kuwasikiliza wanasiasa waliokuwa wakiwahamasisha kukataa bila
kujua faida ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami sasa wajiandai kuitunza
itakapo kamilika na kukabidhiwa”alisema.
Aidha Kadashi alisema kwamba mradi huo utakuwa na manufaa sana kwa
Jiji la Mwanza kutokana na changamoto iliyopo ya musongamano wa magari makubwa
ya mizigo na abiria kufika katikati ya Jiji na yale yanayopita kwenda maeneo
mengine, barabara hiyo ikikamilika utakuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa
msongamano uliopo kwa sasa na kuwa njia ya mkato kwa kuelekea Magu na Misungwi
na Kigongo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Fera kinachopitiwa na
barabara hiyo Leonarld Mongo alisema kwamba wanaipongeza serikali ya awamu ya
nne ya Rais Dkt. Kwa kutekeleza ahadi kwa vitendo ya ujenzi wa barabara hiyo
kama ilivyowaahidi wananchi wa Wilaya hizo mbili na kutambua umuhimu wa kuwa
kuwapatia maendeleo wananchi wake ikiwa na lengo la kuwarahisishia usafiri.
Sehemu ambapo kunajengwa daraja la kivuko cha juu kwa waendao kwa miguu shughuli za ujenzi zinaendelea ndani, nao ujenzi ukitarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwaka 2014. |
Upanuzi wa barabara ya Nyerere inayounganisha njia kuelekea Musoma mkoani Mara, unakwenda sambamba na utanuzi wa madaraja yote ya njia hiyo ili kuendana na vipimo vya upana wa barabara. |
Bango la mkandarasi ambapo juu linaloonyesha mchoro wa jinsi daraja la Mabatini litakavyokuwa. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.