ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 15, 2013

DIWANI CHADEMA APONGEZA KAZI ZA MAENDELEO ZINAZOFANYWA NA MBUNGE WA CCM

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo akikagua baadhi ya majengo katika ziara yake ya kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni kwake..

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa kada mbalimbali kukagua majengo katika ziara yake ya kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni kwake..

Muonekano wa baadhi ya majengo ambayo ujenzi unaendelea..

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo akitoa angalizo juu ya kutimiza wajibu kwa viongozi pamoja na kutunza rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na kuzingatia suala la utawala bora.

DIWANI wa Kata ya Tai kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Rorya Godfrey Masiroli amesifia jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Lameck Airo kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo jimboni na kudai ni Mbunge wa vitendo na sio kuongea.

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge huyo Kijiji cha Sota baada ya ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo za Jimbo hilo na kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Majengo iliyopo katika Kata hiyo baada ya kuezuliwa na upepo.

Alisema Mbunge huyo amekuwa ni mwepesi wa kujitoa na kushiriki mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jimbo na pale yanapotokea majanga amekuwa akifika kwa wakati na kushirikiana na Wananchi ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo.

Masiroli alisema harambee iliyofanywa na Mbunge huyo katika mkutano wa hadhara japo ni ya kushitukiza lakini inaonyesha ni jinsi gani anavyoguswa na Wananchi wa Rorya na kutaka majengo yaliyoezuliwa na upepo yaweze kukamilika na wanafunzi waendelee na masomo.

"Ndugu zangu hii shule ni yetu na wanafunzi wanaosoma hapa ni wetu naungana na mbunge kwa kuchangia shilingi laki moja ili shule hii iweze kukamilika kwa wakati na vijana wetu waendelee na masomo.

"Katika suala shughuli za Maendeleo itikadi za kisiasa tunaweka pembeni na kwa pamoja tunashiriki shughuli za kimaendeleo jambo hili linalofanywa na Mbunge ni jambo jema na kila mmoja ana kila sababu ya kusifia jambo hili,"alisema Masiroli.

Akizungumza katika mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo alisema aliguswa na taarifa ya kuezuliwa kwa shule hiyo akiwa katika vikao vya Bunge na kuamua kuaga ili kuweza kushiriki moja kwa moja katika tatizo hilo.

"Ndugu zangu niliguswa na suala hili na kuamua kuaga bungeni lakini kabla sijafika hapa tayari niliagiza mafundi kuja kuangalia athari iliyopatikana hapa na kuanza kwa ujenzi,lakini kazi hii inapaswa kushikiana na kila mwana Rorya na mdau wa elimu ili vijana wetu waendelee kusoma.

"Sasa hivi suala la elimu ndio linaloangaliwa katika kila sehemu,lazima majengo haya yakamilike na watoto wetu wasome naomba kila mmoja aje kuchangia ili madarasa haya yaliyoezuliwa yaweze kukamilika,"alisema Lameck.

Katika harambee hiyo ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vilivyoezuliwa na upepo iliyoongozwa na Mbunge huyo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana zikiwemo ahadi ya mifuko 19 ya saruji.
CHANZO: BINDA NEWS - MARA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.