Thursday, August 15, 2013
Taarifa kwa vyombo vya
habari
Yah:- Kukabidhiwa vifaa vya mazoezi na nauli wachezaji wa timu ya taifa ya
ngumi.
Mkurugenzi wa
St. Merry School na New Palm Hotel iliyopo Bagamoyo, Ndugu
Mutta Rwakatale kesho ijumaa, saa 6.30 Mchana katika ofisi za Shirikisho la
Ngumi Tanzania (BFT) zilizopo karibu na uwanja wa ndani wa Taifa (indoor
stadium) atatoa vifaa vya mazoezi na
nauli kwa wachezaji wa timu ya taifa inayofanya mazoezi uwanja wa taifa wa
ndani kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa,
tukianzia kushiriki mashindano ya
ubingwa wa Afrika yatakayofanyika kuanzia Sept. 01-07/2013 nchini Mauritius,
Mashindano ya Jumuiya ya Madola 2014, Mashindano ya Afrika 2015 Mashindano ya
Olimpiki 2016 na mengine mengi.
BFT tumefurahishwa mno na mwitikio wa Mkurugenzi huyo kwa
kusikia na kuguswa kuhusu timu ya taifa ya ngumi na BFT tunaona msaada huo umekuja kwa muda mwafaka kwa kuwa
timu yetu ya taifa inafanya mazoezi
katika hali duni, kwa kutumia vifaa ambavyo vimechakaa, lakini pia wachezaji walikuwa
wanafika mazoezini kwa kujitolea wao kama wao kwa nauli zao, hivyo tunaamini
msaada huo utaleta hamasa zaidi kwa wachezaji kipindi hiki kilichobakia kabla
ya kwenda kushiriki mashindano ya ubingwa wa Afrika nchini Mauritius, kwani
tunaamini sasa ratiba ya makocha itafanyika kama walivyopanga na wachezaji
wataweza kufika wote mazoezini na kwa wakati.
BFT tunawaomba watanzania wengine wajitokeze zaidi kusaidia
timu yetu ya taifa ili uwakilishi katika mashindano ya kimatifa uwe wenye tija.kwa
kuzingatia kuwa watanzania wote ndio wanachohitaji na ili kitimie mabondia
lazima tuwaandae vema.
Pia naomba sana
vyombo mbalimbali vya habari kujitokeza katika hafla hiyo fupi kwa nia ya
kuhamasisha ili watanzania wengine kujitokeza kuendelea kusaida zaidi maana
bado msaada unahitajika wa vifaa vya mazoezi, matibabu, chakula, maji,nauli,
nguo za mazoezi na posho
KATIBU MKUU.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.