Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Bw. Ernest Mangu amesema kuwa tukio hilo lilitokea Agust 12 majira ya saa tatu usiku jijini hapa. (KUMSIKILIZA BOFYA PLAY)
Kamanda Mangu ameongeza kuwa idadi ya majambazi hao haikuweza kufahamika na walikuwa na bunduki aina ya SMG yenye namba 2916 na risasi saba ambazo hazijatumika.
Amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu tukio lililopangwa kuvamia kituo hicho, aliagiza askari wake kuweka doria eneo la tukio ambapo waliweza kupambana na majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwauwa watatu kati yao huku wengine wakifanikiwa kutokomea kusikojulikana.
"Inasemekana kuwa majambazi hao walitokea wilayani Ngara mkoa wa Kagera na silaha waliyokuwanayo ina namba tofauti na za Tanzania" Alisema Kamanda Mangu na kudai kuwa huenda wakawa ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Miili ya majambazi hao ilipelekwa hospitali ya Bugando na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kuwabaini majambazi wengine waliotoroka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.