ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 14, 2013

PAMBA SPORTS CLUB YACHUKUWA WANNE TOKA RORYA

Mbunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara Mhe. Lameck Airo akizungumza na wachezaji wa kombaini ya jimbo lake katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao iliyofanyika katika Hotel Lakairo jijini Mwanza ambapo timu hiyo ilifanya ziara ya mechi za kujipima nguvu kwa miji ya Mwanza, Geita na Kahama ikiwa ni fursa kwa vijana wa timu hiyo kutangaza vipaji walivyonavyo kwa timu nyingine kanda ya ziwa hasa kwa msimu huu wa usajili. 


Mhe. Lameck amewasihi vijana hao wa jimbo lake kulipa kipaumbele suala la nidhamu kwa mchezo waliouchagua ambao ndiyo ajira yao, ratiba ya shughuli zote za soka kuanzia mazoezini hadi mtaani kwenye maisha ya kila siku. 


Pichani Mhe. Lameck Airo akiwa katika picha ya pamoja na vijana wanne wenye vipaji walifuatiliwa kwa ukaribu kupitia michezo yao ya kirafiki waliyocheza kanda ya ziwa na kusajiliwa na Pamba Sport Club ya jijini Mwanza. Rorya ina historia kubwa ya kutoa wachezaji wengi maarufu waliyo ichezea Pamba na Toto, mfano mzuri ni Athuman Bilali mchezaji wa zamani wa Pamba na sasa ni kocha wa Toto Africans. Na wengine wengi ambao wengine walizichezea Simba na Yanga


Kapteni wa timu hiyo Mageka Samuel alitoa shukurani za dhati kwa niaba ya timu kwa Mhe. Lameck pamoja  wafanyakazi wote wa Lakairo Investment kwa ukarimu waliouonyesha kwao mwanzo wa safari hadi usiku wa hafla.


Chakula kikiendelea kwenye hafla hiyo.


Viongozi wa timu na wadhamini.


Smile kubwaaaaa....!!!!


Mbunge wa Rorya Lameck Airo (kushoto) akiwa na mmoja kati ya vijana waliosajiliwa Pamba Sports Club (katikati) na kulia ni mkuu wa msafara Mwl. Jamoko Katete. 


Hafla ikiendelea na mivinyo moto kwa baridi..


Mr. Otieno Airo naye alipata fursa ya kuzungumza kwa ukaribu na vijana hao wa Kombaini ya Rorya ambao walidhuru kanda ya ziwa kwaajili ya mazoezi na kufungua fursa za kusajiliwa timu mbalimbali.


Mheshimiwa Lameck Airo akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 3.8 kwa timu hiyo, ambapo kiasi hicho kiligawanywa kwa kila mchezaji, kocha na kiongozi msafara kwa uwiano sawa bila kujali nani ni nani. Fedha hizo zilichangwa na wadau wa karibu wanaomsapoti Mbunge wa Rorya.


Jason Gosbert akikumbusha moja kati ya matukio yakuchekesha yaliyojitokeza kwenye ziara ya vijana hao. 


Nkabaaaa mafungu mezani...


Tofauti na miaka yote iliyopita kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara kuwa na mashiko pekee kwa wadau wengi hapa nchini kufuatilia hatua kwa hatua mwenendo wake, safari hii ya msimu wa ligi 2013-2014, dalili zimeanza kuonekana kuwa nayo ligi soka daraja la kwanza itazoa wengi mashabiki wafuatiliaji.

Hii ni kutokana na mvutano wa kiushindani unaoonekana katika usajili baina ya timu mbili za Kanda ya ziwa za Pamba Sports Club na Toto Africans, kila timu ikijizatiti kuunda kikosi kitakachoipa ushindi hatimaye kurejea ligi kuu.

Mbali na mashabiki kuanza kuonyesha dalili za kuwa na shauku ya kujua nani na nani kasajiliwa ndani ya vikosi vya Toto na Pamba chagizo jingine ni timu hizo na nyingine kadhaa zenye majina kutinga kwenye ligi hiyo huku wadau wa soka, wafanyabiashara na wakuu wa mikoa husika kuonekana kuhamasika na kuweka nguvu zaidi kuzisaidia timu zao kujiimarisha kiusajili kama tukio la Mhe. Lameck kuhusishwa na usajili wa Pamba lilivyofanyika.


Wakufunzi wa masuala ya michezo waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Mbunge wa Rorya Mhe.Lameck Airo na kufanyika katika ukumbi mdogo wa Hoteli Lakairo iliyopo Kirumba wilayani Ilemela jijini Mwanza.


Hafla hiyo ilihitimishwa kwa sala.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.